Mizigo ifuatayo inaruhusiwa inapoingizwa nchini kama mizigo ya mkazi anayerejea nchini ambaye amefikia umri wa miaka 18:

(a)  mavazi;

(b)   Vifaa binafsi na vya nyumbani vya aina yoyote ambavyo alikuwa anatumia binafsi au katika makazi yake ya awali;

(c) Chombo cha moto,"(ukiondoa mabasi na mabasi madogo yenye uwezo wa kubeba abiria zaidi ya 13  na magari ya mizigo yenye uwezo wa kubeba mzigo zaidi ya tani mbili. Aidha, chombo hicho cha moto kisiwe kimetumika miaka 8 au zaidi tangu kilipotengenezwa na kiwe na ukubwa wa injini usiozidi cc 3000) na kimemilikiwa binafsi na msafiri huyo na amekitumia nje ya Tanzania kwa takriban miezi 12 (ukiondoa  kipindi cha usafirishaji  hususani kama kilisafirishwa kwa meli).