Lengo la mfumo huu ni kusimamia na kudhibiti utoaji wa leseni za udereva kwa ajili ya kutatua tatizo la leseni feki ambazo ni chanzo cha ajali nyingi za barabarani. Hii ni kwa sababu mfumo huu unamruhusu kila mtu kupata leseni yoyote na kuendesha gari lolote analopenda. Hata hivyo, katika mfumo wa sasa, wamiliki wa leseni za udereva za daraja fulani watatakiwa kuendesha magari ya daraja hilo tu ambalo walifanyiwa majaribio na si vinginevyo. Katika hatua ya awali, mwombaji atatakiwa kufanyiwa vipimo vya kibiometriki na kuchukuliwa alama za vidole.