Tamko Kabla ya Mzigo Kufika ni Nini?

Tamko Kabla ya Mzigo Kufika ni mfumo unaotumiwa na Idara ya Forodha na ushuru kuchakata nyaraka muhimu wakati wa kutoa mizigo. Hata hivyo, mchakato wa awali unaanza na mwingizaji wa mzigo kupitia Wakala wake wa Kupokea na Kusafirisha Mizigo aliyeteuliwa.

Angalizo: Ofisi zifuatazo hazitapitia  Mchakato wa kutoa Tamko Kabla ya Mzigo Kufika

 • Mizigo ya Kidiplomasia
 • Fomu za Kujaza Mizigo ya Raia wenye sifa wanaorejea nchini
 • Huduma za Vifurushi vya Posta na usafirishaji wa vifurushi
 • Masuala ya Zanzibar
 • Uingizaji Mizigo Nchini kwa Muda
 • Nyaraka za Kanda Maalum za Uwekezaji
 • Matamko ya kusafirisha Mizigo Nje ya Nchi
 • Bidhaa za Petroli
 • Bidhaa zilizopokelewa chini ya Hati ya Muda
 • Matamko ya Mizigo Inayopitishwa Kwenda Nchi Nyingine

Mtu aliyeagiza bidhaa anapaswa kumpatia Wakala wa Kupokea na Kusafirisha Mizigo nyaraka za kuagiza nje mzigo kwa mkono au kielektroniki ambapo atapakia nyaraka hizo kwenye mfumo wa Tamko Kabla ya Kuwasili Bidhaa na kupeleka nyaraka hizo TRA; ambapo namba ya kumbukumbu itatolewa moja kwa moja na mfumo huo; hizi ni pamoja na:

 • Ankara ya Mwisho
 • Fomu ya Tamko C 36
 • Barua ya Kumwidhinisha Wakala
 • Vibali za kuingiza bidhaa, yaani Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania, Shirika la Viwango Tanzania, kibali cha kemikali, nk
 • Nyaraka za msamaha wa kodi
 • Orodha ya Kufungasha
 • Nyaraka za usafirishaji wa mzigo, yaani Hati ya Kupokea Mzigo Bandarini/Hati ya Kupokea Mzigo Uwanja wa Ndege/Hati ya Taarifa za mzigo Uliosafirishwa kwa njia ya barabara
 •  Hati ya TIN (mtu anayeingiza mzigo)

Angalizo: Nakala za Ankara Kifani zinazosomeka zitapokelewa kwa ajili ya uhakiki na usajili tu lakini si kwa ajili ya kutoa ripoti ya uthibitisho wa malipo (Makadirio ya Awali ya Tamko Kabla ya Mzigo Kufika, Makadirio Halisi ya Tamko Kabla ya Mzigo Kufika nk.)

Angalizo: Vituo vingine vya sasa isipokuwa Dar es Salaam na Tunduma

TRA itahakiki maombi ya Tamko Kabla ya Mzigo Kufika lililowasilishwa ili kuhakikisha kuwa limekamilika, halali na linakubalika kwa kusajili namba zilizotolewa baada ya kuwasilishwa na wakala. Taarifa ya baruapepe itatumwa kiotomati kwa Wakala wa Kupokea na Kusafirisha Mizigo.

 • TRA inafanya kazi ya Kuainisha na Kuthaminisha Viwango vya Forodha na kutoa Makadirio ya Awali ya Tamko Kabla ya Mzigo Kufika kwa waliosajiliwa na Tamko Kabla ya Mzigo Kufika na seti kamili ya nyaraka za mwisho. Tamko Kabla ya Mzigo Kufika llilosajiliwa na seti isiyo kamili ya nyaraka za mwisho inawekwa kusubiri uwasilishaji wa nyaraka kamili.
 • TRA inatoa Makadirio ya Awali ya Tamko Kabla ya Mzigo Kufika ambayo yanapatikana kwa kupakuliwa na Wakala wa Kupokea na Kusafirisha Mizigo kutoka mtandao wa TRA wa Tamko Kabla ya Mzigo Kufika kwa ajili ya kupitia.
 • Wakala anatakiwa kumpatia mwingizaji mzigo Makadirio ya Awali ya Tamko Kabla ya Mzigo Kufika ili aipitie na kukagua usahihi ili aridhie au kukataa Makadirio ya Awali ya Tamko Kabla ya Mzigo Kufika kupitia Mfumo wa Maulizo wa Ndani
 • Iwapo Makadirio ya Awali ya Tamko Kabla ya Mzigo Kufika yatakubaliwa na mwingizaji mzigo; Wakala wa Kupokea na Kusafirisha Mizigo ataomba Makadirio Halisi ya Tamko Kabla ya Mzigo Kufika kupitia www.trapad.co.tz pamoja na nyaraka zilizoskaniwa kama inavyotakkiwa, kama vile vibali na/au hati zilizotolewa na Idara Nyingine za Serikali (Shirika la Viwango Tanzania, Mkemia Mkuu wa Serikali, Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania, nk.) na nyaraka za kuthibitisha misamaha ya kodi, kama ipo.
 • TRA itahakiki maombi na kutoa Makadirio ya Tamko Kabla ya Mzigo Kufika (Makadirio Halisi ya Tamko Kabla ya Mzigo Kufika) yaliyopo kwa ajili ya kupakuliwa na Wakala wa Kupokea na Kusafirisha  Mizigo kutoka tovuti hii. Baruapepe ya taarifa itatumwa moja kwa moja kwa Wakala wa Kutoa na Kusafirisha Mizigo.
 • Data ya Makadirio Halisi ya Tamko Kabla ya Mzigo Kufika EDI inapatikana kwa ajili ya kupakuliwa na Wakala wa Kutoa na Kusafirisha Mizigo kutoka tovuti hii kwa ajili ya kupakia kwa msingi wa Makadirio Halisi ya Tamko Kabla ya Mzigo Kufika iliyotolewa. Wakala wa Kupokea na Kusafirisha Mizigo atakadiria Ushuru na Kodi kupitia Waraka Mmoja Wa Usimamizi Tanzania
 • Wakala atakabidhi Waraka Mmoja Wa Usimamizi Tanzania kwa mwingizaji mizigo tayari kwa ajili ya kulipia ushuru na kodi Benki.
 • TRA inafanya mchakato wa kuchagua kwa kuingiza Waraka Mmoja Wa Usimamizi Tanzania kwenye Mfumo wa Kikompyuta wa Udhibiti wa Hatari; kwa kuzingatia matokeo.

 

Angalizo: Rangi ya KIJANI inaashiria kuruhusu moja kwa moja wakati MANJANO kukagua nyaraka/KUSKANI na NYEKUNDU ukaguzi wa kiupekuzi au kuskani.

 

 • Bidhaa zikishakaguliwa zinaruhusiwa kutoka Bandarini au Uwanja wa Ndege

Angalizo: Kwa watumiaji wa Mfumo wa Pamoja wa Forodha Tanzania (Kwa sasa upo Dar es Salaam na Tunduma)

 • Iwapo tamko “Limekataliwa” Wakala wa Kupokea na Kusafirisha Mizigo anatakiwa kuwasilisha tamko jipya linalozingatia masharti ya Mfumo wa Pamoja wa Forodha Tanzania.
 • Waraka Mmoja wa Usimamizi Tanzania utachakatwa katika hatua ya malipo kabla ya orodha ya shehena kuwasilishwa.
 • Orodha ya Shehena iliyokwisha inabadilishwa kwenda katika hatua ya Agizo la Ruhusa ya Forodha.
 • Wakala wa Kupokea na Kusafirisha Mizigo atapata Taarifa ya Kukubaliwa pamoja na Taarifa ya Malipo iliyoandaliwa kwa kuzingatia Thamani iliyotajwa.
 • Wakala wa Kupokea na Kusafirisha Mizigo atapata Taarifa ya Kukubaliwa  kwa Marekebisho mara marekebisho waliyotuma yanapokuwa yamepitia ukaguzi wa marekebisho. Iwapo afisa amebatilisha marekebisho Wakala wa Kupokea na Kusafirisha Mizigo atapata Taarifa ya Kukataliwa kwa Marekebisho ya Waraka Mmoja Wa Usimamizi Tanzania; vinginevyo afisa huyo atashughulika na kuainisha, kuthaminisha na kuthibitisha waraka.
 • Mara uhakiki unapokuwa umekamilika, matokeo yatasajiliwa na afisa husika.
 • Matokeo ya uhakiki yatawasilishwa kwa msimamizi kwa  ajili ya kuidhinishwa.
 • Wakala wa Kupokea na Kusafirisha Mizigo atapokea Taarifa za Makadirio.
 • Wakala wa Kupokea na Kusafirisha Mizigo anapaswa kukubali au kupinga Taarifa ya Makadirio
 • Wakala wa Kupokea na Kusafirisha Mizigo anapaswa kupinga Makadirio ya Afisa kupitia Mfumo wa Pamoja wa Maulizo
 • Iwapo Wakala wa Kupokea na Kusafirisha Mizigo anakubali Taarifa na makadirio yameongozeka ikilinganishwa na thamani iliyotajwa, Taarifa ya Malipo ya Ziada itatolewa ndani ya taarifa ya makadirio. Taarifa hii ya thamani ya malipo itakuwa tofauti ya kiasi cha mwisho na taarifa ya malipo iliyotolewa awali.
 • Iwapo kutakuwa na tofauti kati ya data ya orodha ya shehena na tamko, Wakala wa Kupokea na Kusafirisha Mizigo atapokea Taarifa ya Kunyimwa Kibali. Wakala wa Kupokea na Kusafirisha Mizigo atapaswa kurekebisha tamko kama atakavyoelekezwa na matokeo ya ukaguzi na kuliwasilisha tena.
 • Malipo yatakapokuwa yamepokelewa, ukaguzi kukamilika ipasavyo, Wakala wa Kupokea na Kusafirisha Mizigo atapokea Kibali cha Kutoa Mzigo husika.

Mchakato huu unachukua muda gani kabla ya kupata mizigo?

 • Jumla ya saa 48 (siku 4) zimepangwa kwa ajili ya kushughulikia Taarifa Kabla ya Kuwasili kwa Mzigo kuanzia usajili hadi utoaji wa ripoti muhimu za kutoa mzigo (Makadirio Halisi ya Tamko Kabla ya Mzigo Kufika) kwa Taarifa Kabla ya Kuwasili kwa Mzigo zilizowasilishwa pamoja na au baada ya kupokea nyaraka za kutosha ambazo zinakidhi viwango vinavyotakiwa.
 • Makadirio ya Awali ya Tamko Kabla ya Mzigo Kufika kwa Taarifa Kabla ya Kuwasili kwa Mzigo zilizowasilishwa pamoja na seti kamili ya nyaraka za mwisho zinapaswa kushughulikiwa na kutolewa ndani ya saa 48.
 •  Angalizo: Makadirio ya Awali ya Tamko Kabla ya Mzigo Kufika kwa Taarifa Kabla ya Kuwasili kwa Mzigo zilizosajiliwa bila seti kamili ya nyaraka za mwisho zinapaswa kushughulikiwa na kutolewa saa 48 baada ya kupokea Taarifa Kabla ya Kuwasili kwa Mzigo, yaani iwapo nyaraka za mwisho zinapokelewa baada ya wiki mbili, mchakato unaanzia siku hiyo.
 • Makadirio Halisi ya Tamko Kabla ya Mzigo Kufika yanapaswa kushughulikiwa na kutolewa ndani ya saa 24 baada ya kupokea maombi ya Makadirio Halisi ya Tamko Kabla ya Mzigo Kufika pamoja na seti kamili ya nyaraka zinazohitajika.
 • Baada ya kujaza Waraka Mmoja Wa Usimamizi Tanzania na malipo ya ushuru kama upo, uchaguzi utafanyika ndani ya saa 24.

Mizigo inateuliwa kwa itakayoruhusiwa kutolewa moja kwa moja, ya kijani itapata kibali cha kutolewa bandarini au mahali pa kuingizia mizigo, ile iliyochaguliwa kwa ajili ya ukaguzi wa nyaraka itakaguliwa katika CSC, na ile iliyochaguliwa kwa ajili ya ukaguzi wa kiupekuzi na kuruhusiwa kutolewa bandarini na mahali pa kuingilia