Utangulizi:

Wakala wa Kupokea na Kusafirisha Mizigo ni watu waliopewa leseni na Kamishna wa Idara ya Forodha na Ushuru kufanya kazi ya kushughulikia nyaraka na kupokea mizigo kutoka kwenye udhibiti wa forodha kwa niaba ya wanaoingiza mizigo.

Masharti gani mtu anatakiwa kutimiza ili kusajiliwa kama Wakala wa Kupokea na Kusafirisha Mizigo?

Maombi yanapaswa kutolewa kwenye fomu ya forodha (Fomu C.20) na iambatishwe na:

1)     Uthibitisho wa malipo ya ada ya maombi – $ 50 za Marekani;

2)     Hati ya usajili Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA);

3)     Uthibitisho wa ushiriki au uanachama kwenye chama cha wapokeaji na wasafirishaji wa mizigo kinachotambulika;

4)     Barua kutoka kwa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) ikieleza hali ya sasa ya Wakurugenzi na Wanahisa wa kampuni;

5)     Uthibitisho wa uanachama kwenye mfuko wa umma wa hifadhi ya jamii kwa kila mwajiriwa wa kampuni.

6)     Dhamana ya benki, iliyoandikwa kwa maslahi ya Kamishna wa Forodha na ushuru, wa angalau shilingi 100,000,000 na ambayo itabaki kuwa hai kwa muda wote wa leseni, yaani tarehe 1 Januari – 31 Desemba 2016 (waombaji wapya wawasilishe dhamana hii baada ya kufaulu mtihani);

7)     Leseni ya Forodha iliyo Hai kwa ajili ya mwaka unaofuata (kwa ajili ya kuongeza muda);

8)     Kwa mwombaji mpya, barua ya utambulisho, nakala mbili, kwa mmoja wa watu wenye sifa katika (8) hapo juu ambaye atawakilisha kampuni kwenye usaili na iwe na anwani ya baruapepe na namba ya simu alimradi anatimiza masharti yafuatayo:

i)      Yeye ni mkurugenzi au mfanyakazi wa kudumu wa kampuni, NA

ii)     Ana Hati ya Forodha ya Afrika Mashariki ya Kufanya Kazi za Kupokea na Kusafirisha Mizigo, NA

iii)    Yeye hajawahi kuwa mkurugenzi wa kampuni ambayo leseni yake ya uwakala wa Forodha imewahi kufutwa;

9)     Hati iliyosainiwa kati ya wakurugenzi wote wa kampuni hakuna aliyewahi kuwa mkurugenzi wa kampuni yenye kibali ambayo leseni yake imefutwa katika miaka mitano iliyopita;

10)  Hati iliyosainiwa ambapo kati ya wakurugenzi wa kampuni hakuna aliye mkurugenzi wa kampuni hai yenye leseni;

11)  Hati iliyosainiwa ambapo kati ya wakurugenzi au wanahisa wa kampuni hakuna aliye mwajiriwa wa TRA;

12)  Hati ya kufanya kazi ya kutoa huduma za msingi za Forodha katika utaratibu wa kazi wa saa 24 na siku saba.

 

Orodha ya Mawakala wa Forodha