Makamu wa Rais afanya mazungumzo na Kamishna Mkuu wa TRA
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere (kulia) akiwa katika kikao na uongozi wa Kiwanda cha kutengeneza vinywaji visivyo na kilevi cha DI & PC kilichopo Jijini Dodoma, wakati alipofanya ziara yake ya kikazi kiwandani hapo kuangalia muitikio juu ya ulipaji kodi na kutatua changamoto zinazowakumba.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere (kulia) akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Kiwanda cha kutengeneza vinywaji visivyo na kilevi cha DI & PC kilichopo Jijini Dodoma, Bibi. Catherine Mwimbe wakitazama miundombinu ya kiwandani hapo wakati wa ziara yake ya kikazi.
Kamishna wa Kodi za Ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Elijah Mwandumbya (kushoto) akiongea na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Alan Kijazi kuhusu ukusanyaji wa kodi katika sekta ya Utalii.
Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu Hasani akiwa anapitia moja ya machapisho yanayohusu kodi alipotembelewa na Kamishna Mkuu wa TRA
Daraja la Kelema linalounganisha barabara kutoka Dodoma kuelekea Babati mkoani Manyara, ujenzi wa daraja hilo umetokana na kodi za Watanzania.
Barabara ya kutoka Dodoma kuelekea Mkoani Iringa kupitia Mtera ikiwa imekamilika na kwa sasa inapitika, ujenzi wa barabara hii unatokana na kodi za Watanzania.
Kivuko kipya cha Msanga Mkuu mkoani Mtwara ambacho kwa sasa kinatumika kuvusha wakazi wa mkoani hapo, ambapo upatikanaji wa kivuko hicho unatokana na kodi za Watanzania

Piga simu bure Tanzania

0800 750 075 

0800 780 078

Namba mbadala:

+255 22-2119343

 Barua Pepe:This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

 Facebook:tratanzania

 Twitter:tratanzania

 Instagram:tratazania