Hii ni kodi inayotozwa kwenye mapato yatokanayo na michezo ya kubahatisha. Kodi hizi ni za aina mbili: -


  • Kodi ya Michezo ya Kubahatisha (Gaming Tax)

     Hii ni kodi anayotozwa mwendeshaji wa mchezo wa kubahatisha kutokana na mapato yake yatokanayo na michezo ya kubahatisha.

  • Kodi ya Michezo ya Kubahatisha kwenye Zawadi (Gaming Tax on Winnings)

Hii ni kodi anayotozwa mchezaji baada ya kushinda zawadi ya mchezo wa kubahatisha.

Aina ya michezo inayotozwa kodi hii: -

(a)  Kasino (Casino)

(b)  Kasino Mtandao

(c)   Kasino ndogo (Mini Casino/Forty machines sites)

(d)  Michezo ya Kubashiri Matokeo (Sports Betting),

(e)  Michezo ya Machine (Slots machines/route operations),

(f)    Bahati Nasibu ya Taifa (National lottery)

(g)  Bahati nasibu ya kutumia ujumbe mfupi wa simu.(SMS lottery)

(h)  Michezo ya Vikaragosi (Virtual Games)

 Viwango vya kodi vinavyotozwa na tarehe ya kulipa kodi

Kodi ya Michezo ya Kubahatisha (Gaming Tax);

Na

Aina ya Mchezo

Viwango vya kodi vinavyotozwa

Tarehe ya kulipa kodi

1

Kasino (Land Based Casino)

18% ya Mapato Ghafi (mauzo baada ya kutoa gharama za ushindi)

12% ya Jumla ya zawadi aliyoshinda Mchezaji

Kila wiki

2

Kasino Mtandao (Internet Casino)

25% ya Mapato Ghafi (Mauzo baada ya kutoa gharama za ushindi)

15% ya Jumla ya zawadi aliyoshinda Mchezaji

 

Kila Mwezi

3

Michezo ya Kubashiri Matokeo (Sports Betting)

25% ya Mapato Ghafi (Mauzo baada ya kutoa gharama za ushindi)

10% ya Jumla ya zawadi aliyoshinda Mchezaji

 

Kila mwezi

4

Bahati nasibu ya kutumia ujumbe mfupi wa simu (SMS Lotteries)

25% ya Mapato Ghafi (Mauzo baada ya kutoa gharama za ushindi)

15% ya Jumla ya zawadi aliyoshinda Mchezaji

 

Kila mwezi

5

Bahati Nasibu ya Taifa (National Lotteries)

20% ya Mapato Ghafi (Mauzo baada ya kutoa gharama za ushindi)

15% ya Jumla ya zawadi aliyoshinda Mchezaji

 

Kila mwezi

6

Kasino ndogo (Forty Machines Sites)

25% ya Mapato Ghafi ya Michezo ya Kwenye Mashine (Mauzo baada ya kutoa gharama za ushindi)

 

Kila mwezi

7

Michezo ya Machine (Slot Machines)

Tshs. 100,000 kwa kila mashine

Kila mwezi

8

Michezo ya Vikaragosi(Virtual Games)

10% ya jumla ya zawadi anayopata Mchezeshaji

15% ya jumla ya zawadi aliyoshinda Mchezaji

Kila mwezi


  

 Takwimu za Fedha za Serikali na Maelezo

Kifungu

Namba ya Takwimu ya Fedha ya Serikali

Maelezo

440

11440107

Michezo ya Kubashiri Matokeo kwenye mapato ghafi

440

11440108

Michezo ya Kubashiri kwa wachezaji

440

11440109

Michezo ya mashine

440

11440110

Bahati Nasibu ya kutumia ujumbe mfupi wa simu

440

11440111

Bahati Nasibu ya Taifa

440

11440112

Mapato ghafi kwenye Kasino

440

11440113

Zawadi  anayopata Mchezaji

440

11440114

Kasino Ndogo

440

11440115

Michezo ya Vikaragosi kwa Mchezeshaji

440

11440116

Mchezo wa Vikaragosi kwenye  zawadi anayopata Mchezaji

 

Walipakodi katika Tasnia ya michezo ya kubahatisha wanaelekezwa yafuatayo:

(a)  Kulipa kodi zitokanazo na michezo ya kubahatisha kwa viwango vilivyowekwa

(b)  Kujisajili na kutapata Namba ya Utambulisho ya  Mlipakodi kama hawajasajiliwa.

(c)   Kujaza na kuwasilisha ritani za kodi za michezo ya kubahatisha katika ofisi za TRA amabazo wamesajiliwa.

(d)  Kujaza GFS sahihi kama zilivyoonyeshwa hapo juu wakati wa kufanya malipo ya kodi ya michezo ya kubahatisha kwa kadri ya mchezo wa kubahatisha ulihusika.

Angalizo:

Vipengele vya Sheria ya Usimamizi wa Kodi kuhusiana na kutunza kumbukumbu, madeni ya kodi, kukusanya na kukomboa kodi, kutoza riba na pingamizi za kodi vitahusika pia katika kutoza na kusimamia kodi ya michezo ya kubahatisha.