Utangulizi

Maduhuli ni bidhaa na huduma zinazoingizwa nchini Tanzania kutoka nje ya nchi. Taratibu za maduhuli zinapaswa kufuatwa ili kukomboa bidhaa kutoka Forodhani kulingana na Sheria ya Usimamizi wa Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya mwaka 2004.

Maduhuli kuja Tanzania yanapitia hatua mbalimbali ambapo mwingizaji anashauriwa kutoa tamko kupitia Wakala wake wa Upokeaji na Usafirishaji wa Mizigo kwa kukabidhi nyaraka angalau siku saba kabla ya kuwasili kwa chombo cha usafirishaji.

Taratibu za Kuingiza bidhaa nchini Tanzania

  • Mwingizaji bidhaa anatakiwa kumteua Wakala wa Kupokea na Kusafirisha Mizigo mwenye Leseni ili aweze kupokea/kukomboa bidhaa zake
  • Orodha ya Wakala wa Kupokea na Kusafirisha Mizigo
  • Mchakato wa kuandikisha unafanyika mtandaoni kupitia Mfumo wa Pamoja wa Forodha Tanzania (TANCIS) kwa upande wa Tanzania bara na mfumo wa ASYCUDA ++ kwa upande wa Zanzibar, fomu zinaweza kujazwa kabla ya bidhaa kuwasili
  • Wakala wa forodha na usafirishaji wa mizigo/waingizaji wa bidhaa wanatakiwa kujaza Tamko na makadirio binafsi kupitia Mfumo wa Pamoja wa Forodha Tanzania (TANCIS)  na ASYCUDA++ kwa upande wa Zanzibar, na kuambatanisha nyaraka nyinginezo husika za kuingiza bidhaa/za uthibitisho angalau siku 7 kabla ya kuwasili kwa bidhaa.

Nyaraka za kuingiza bidhaa zinajumuisha

  • Ankara ya Mwisho
  • Barua ya Kumwidhinisha Wakala kutoka kwa mwingizaji mzigo
  • Vibali vya kuingiza bidhaa kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania, Shirika la Viwango Tanzania, nk
  • Nyaraka za msamaha wa kodi (Kama zipo)
  • Orodha ya Ufungashaji
  • Nyaraka za usafirishaji, yaani Hati ya Kupokea Mzigo Bandarini/Hati ya Kupokea Mzigo Uwanja wa Ndege/Taarifa za mzigo uliosafirishwa kwa njia ya barabara

Taarifa kuhusu Fedha Taslimu na Hati za Malipo zinazosafirishwa kuingia au kutoka nje ya Nchi

Angalizo

Mfumo wa uondoshaji mizigo hautakubali tamko ambalo halijakamilika au lenye maelezo pungufu kupitia katika mfumo wake wa maulizo ambao unapatikana katika mfumo wa pamoja wa forodha Tanzania (TANCIS).