Utangulizi

Mtu ambaye ni raia nje ya jumuiya ambaye anatarajia kuingiza bidhaa ambazo zitakaa kwa muda mfupi katika nchi wanachama ataingiza bidhaa bure kwa kuzingatia bidhaa hizo zitaondoshwa tena.

 

Bidhaa ambazo zinaingizwa kwa dhumuni la matumizi ya muda mfupi zinajumuisha:

a)    sampuli za wasafiri za kibiashara

b)    Bidhaa, ikiwemo vifaa kwa ajili ya kutengeneza jukwaa, inayoingizwa kwa ajili ya Maonesho au burudani

c)    Bidhaa zinazoingizwa kwa ajili ya ukarabati na matengenezo

d)    Bidhaa za uendelezaji utalii ambazo hazijapigwa marufuku

e)    Magari yote na bidhaa zinazoingizwa na raia aliye chini ya COMESA au SADC au Jumuiya ya Afrika Mashariki.

 

Mtu ambaye anatarajia kuingiza bidhaa kwa muda mfupi anapaswa kufanya maombi kwa kujaza fomu namba C.17 (TANCIS) na maombi hayo yaeleze;

a)    Taarifa kamili ya mzigo unaoingizwa, ueleze asili ya bidhaa na dhumuni lake, utambulisho; na

b)    Makadirio ya tarehe na mahali ambapo mzigo utaondoshwa, pia mwingizaji anatakiwa kuweka kiasi ambacho kitakachotosheleza kodi ya bidhaa hiyo au awekeze dhamana katika Maghara ya Dhamana ya Forodha na afisa atathibitisha. 

 

KUMBUKA:

Afisa atapitia maombi ya mmliki, na ataeleza kiasi cha kodi ambacho kinapaswa kutozwa, na kiasi cha kuweka kama dhamana.

Kama bidhaa zitakuwa za kuondoshwa katika mahali ambapo ni tofauti na mahali alipoingizia bidhaa, maombi yatafanyika katika nakala tatu.

Kama Afisa atahitaji, Ankara au nyaraka ambazo zitaonesha uwalali wa thamani ya bidhaa, mwingizaji anapaswa kuambatanisha kwenye maombi yake.

Magari na bidhaa zinazoingizwa zinapaswa kuondoshwa ndani ya kipindi cha miezi kumi na mbili kutokea tarehe ya kuingiza mzigo.