Kuelewa dhana ya Kodi inayotokana na Ajira
Kodi inayotokana na Ajira inajulikana kama Lipa kadiri unavyopata. Hii ni kodi ya zuio kwa waajiriwa wanaotozwa kodi. Chini ya mfumo huu, mwajiri anapaswa kisheria kukata kodi ya mapato kutoka katika mshahara au ujira wa mwajiriwa anayestahili kutozwa kodi.
Maana ya Mwajiriwa:
Mwajiriwa ni mtu anayehusika na ajira inayoendeshwa na mwajiri. Ajira inahusisha waajiriwa wa kudumu, waajiriwa wa muda, meneja, Mkurugenzi, na vibarua. Waajiriwa wanaweza kuajiriwa na mwajiri mmoja au zaidi (ajira ya msingi na ya ziada)
Maana ya mwajiri:
Mwajiri ni mtu anayeendesha, aliyeendesha au ana lengo la kuendesha ajira kwa watu.
Mkurugenzi wa ajira ya kudumu:
Maana yake ni mwajiriwa wa kudumu katika shirika anayefanya kazi ya kiutawala.
Usimamizi wa Kodi ya Mshahara
Mwajiri anapaswa kuzuia kodi ya mapato kutoka katika mishahara, ujira na malipo mengine yote yanayopaswa kukatwa kodi kutoka kwa waajiriwa.