Sheria inayosimamia Pingamizi na Rufaa za Kodi
Pingamizi na rufaa zinasimamiwa na Sheria ya Rufaa ya Kodi Kifungu Na.408 na marekebisho yake mara kwa mara.
Utangulizi kuhusu Pingamizi na Rufaa
Sheria za Kodi Tanzania inamruhusu mtu yeyote anayehisi kuwa amenyimwa haki kuomba mabadiliko rasmi ya maamuzi rasmi kuhusiana na makadirio ya kodi yaliyofanywa na Kamishna Mkuu. Mlipakodi anayehisi kuwa Kamishna Mkuu ametumia vibaya sheria, amefikia kupata matokeo ambayo si sahihi, alitumia vibaya mamlaka yake, alikuwa na upendeleo, alizingatia ushahidi ambao hakupaswa kuuzingatia au ameshindwa kuzingatia ushahidi ambao angepaswa kuuzingatia katika kufanya makadirio ya kodi, anaweza kupinga makadirio hayo.