Mamlaka ya Mapato Tanzania imetoa kalenda hii ili kuwakumbusha walipakodi na wadau tarehe muhimu za kujaza taarifa za malipo ya kodi, kufanya malipo ya kodi na matukio mengine muhimu. Kalenda hii itawasaidia katika kupanga masuala yenu ya kodi.

Tarehe

Suala/Tukio

Ijumaa,7 Januari

Tarehe ya kulipa Kodi ya Mshahara, Kodi ya Kuendeleza Ujuzi na kodi nyingine za zuio chini ya Kodi ya Mapato

Alhamisi, 20 Januari

Tarehe ya kuwasilisha Ripoti za VAT za Desemba 2020  na kulipa kodi kulingana na ripoti

Jumatano, 26 Januari

Siku ya Forodha Duniani

Jumatatu, 7  Februari

Tarehe ya kulipa Kodi ya Mshahara, Kodi ya Kuendeleza Ujuzi na kodi nyingine za zuio chini ya Kodi ya Mapato

Jumatatu, 21 Februari

Tarehe ya kuwasilisha Ripoti ya VAT na kulipa kodi kulingana na ripoti

Jumatatu, 7  Machi

Tarehe ya kulipa Kodi ya Mshahara, Kodi ya Kuendeleza Ujuzi na kodi nyingine za zuio chini ya Kodi ya Mapato

Jumatatu,21  Machi

Tarehe ya kuwasilisha Ripoti ya VAT ya Februari na kulipa kodi kulingana na ripoti ya kodi

Alhamisi, 31  Machi

Walipakodi ya Mapato kwa Awamu:

Tarehe ya malipo ya awamu ya kwanza ya makadirio ya kodi kwa mwaka wa mapato wa 2022  kwa walipakodi ambao kipindi cha hesabu kinaishia Desemba 2022

 Tarehe ya malipo ya awamu ya nne ya makadirio ya kodi kwa mwaka wa mapato wa 2021  kwa walipakodi ambao kipindi cha malipo ya kodi kinaishia Machi 2022

Tarehe ya malipo ya awamu ya tatu ya makadirio ya kodi kwa mwaka wa mapato wa 2022  kwa walipakodi ambao kipindi cha malipo ya kodi kinaishia Juni 2022

Tarehe ya malipo ya awamu ya pili ya makadirio ya kodi kwa mwaka wa mapato wa 2021 kwa walipakodi ambao kipindi cha malipo ya kodi kinaishia Septemba 2022

Alhamisi,31  Machi

Ripoti ya mwisho ya mapato na malipo ya makadirio binafsi ya kodi

 Tarehe ya kuwasilisha ripoti ya mwisho ya mapato kwa mwaka wa mapato wa kwa walipakodi ambao kipindi cha kulipa kodi 2020  kinaishia Septemba 2021

Alhamisi,7  Aprili

Tarehe ya kulipa Kodi ya Mshahara, Kodi ya Kuendeleza Ujuzi na kodi nyingine za zuio chini ya Kodi ya Mapato

Jumatano,20  Aprili

Tarehe ya kuwasilisha Taarifa za VAT za Machi na kulipa kodi kulingana na ripoti

Jumamosi, 7  Mei

Tarehe ya kulipa Kodi ya Mshahara, Kodi ya Kuendeleza Ujuzi na kodi nyingine za zuio chini ya Kodi ya Mapato

Ijumaa, 20   Mei

Tarehe ya kuwasilisha Taarifa za VAT za Aprili na kulipa kodi kulingana na taarifa za kodi

Jumanne, 7 Juni

Tarehe ya kulipa Kodi ya Mshahara, Kodi ya Kuendeleza Ujuzi na kodi nyingine za zuio chini ya Kodi ya Mapato

Jumatatu,20  Juni

Tarehe ya kuwasilisha taarifa ya VAT ya mwezi Mei na kulipa kodi kulingana na taarifa ya mapato

Jumapili,26 Juni

Siku ya madawa haramu Duniani

Alhamisi,30  Juni

Walipakodi kwa awamu:

 Tarehe ya malipo ya awamu ya pili ya makadirio ya kodi kwa mwaka wa mapato  2022  kwa walipa kodi ambao kipindi chao cha malipo ya kodi kinaishia Desemba 2022

 Tarehe ya malipo ya awamu ya tatu ya makadirio ya kodi kwa mwaka wa mapato wa 2022  kwa walipa kodi ambao kipindi cha malipo ya kodi kinaishia Septemba  2022.

 Tarehe ya malipo ya awamu ya nne ya makadirio ya kodi kwa mwaka wa mapato wa 2022 kwa walipa kodi ambao kipindi cha malipo ya kodi kinaishia Juni 2022.

Tarehe ya malipo ya awamu ya kwanza ya makadirio ya kodi kwa mwaka wa mapato wa 2023 kwa walipa kodi ambao kipindi cha malipo ya kodi kinaishia  Machi 2023.

Alhamisi, 30 Juni

Taarifa ya mwisho ya mapato na malipo ya makadirio binafsi ya kodi

Tarehe ya kuwasilisha taarifa ya mwisho ya mapato kwa mwaka 2021  kwa walipa kodi ambao kipindi cha malipo ya kodi kinaishia Desemba 2021.

Alhamisi, 7  Julai

Tarehe ya kulipa Kodi ya Mapato ya Mshahara, Kodi ya Kuendeleza Ujuzi na kodi nyingine za zuio chini ya Kodi ya Mapato

Jumatano, 20 Julai

Tarehe ya kuwasilisha Taarifa za VAT na kulipa kodi kulingana na taarifa za mapato

Jumapili, 7  Agosti

Tarehe ya kulipa Kodi ya Mapato ya Mshahara, Kodi ya Kuendeleza Ujuzi na kodi nyingine za zuio chini ya Kodi ya Mapato

Jumatatu, 22  Agosti

Tarehe ya kuwasilisha Taarifa za VAT za Julai na kulipa kodi kulingana na taarifa ya mapato

Jumatano, 7  Septemba

Tarehe ya kulipa Kodi ya Mapato ya Mshahara, Kodi ya Kuendeleza Ujuzi na kodi nyingine za zuio chini ya Kodi ya Mapato

Jumanne,20 Septemba

Tarehe ya kuwasilisha Taarifa za VAT za Agosti na kulipa kodi kulingana na taarifa za mapato

Ijumaa, 30  Septemba

Walipakodi kwa awamu:

 Tarehe ya malipo ya awamu ya tatu ya makadirio ya kodi kwa mwaka wa mapato wa  2022  kwa walipakodi ambao kipindi cha malipo ya kodi kinaishia Desemba 2022.

Tarehe ya malipo ya awamu ya nne ya makadirio ya kodi kwa mwaka wa mapato wa 2022 kwa walipakodi ambao kipindi cha malipo ya kodi kinaishia Septemba  2022.

 Tarehe ya malipo ya awamu ya kwanza ya makadirio ya kodi kwa mwaka wa mapato wa 2023 kwa walipakodi ambao kipindi chao cha kulipa kodi kinaishia Juni 2023.

 Tarehe ya malipo ya awamu ya pili ya makadirio ya kodi kwa mwaka wa mapato wa 2023  kwa walipakodi ambao kipindi cha kulipa kodi kinaishia  Machi 2023.

Ijumaa, 30  Septemba

Ripoti ya mwisho ya mapato na malipo ya kodi za kujikadiria

Tarehe ya kuwasilisha ripoti ya mwisho ya kodi kwa mwaka wa mapato wa 2021  kwa walipakodi ambao kipindi cha malipo ya kodi kinaishia Machi 2022.

Ijumaa, 7  Oktoba

Tarehe ya kulipa Kodi ya Mapato ya Mshahara, Kodi ya Kuendeleza Ujuzi na kodi nyingine za zuio chini ya Kodi ya Mapato

Alhamisi, 20  Oktoba

Tarehe ya kuwasilisha Taarifa ya VAT ya Septemba na kulipa kodi kulingana na taarifa ya mapato

Jumatatu, 7  Novemba

Tarehe ya kulipa Kodi ya Mapato ya Mshahara, Kodi ya Kuendeleza Ujuzi na kodi nyingine za zuio chini ya Kodi ya Mapato

Jumatatu,21  Novemba

Tarehe ya kuwasilisha Taarifa ya VAT ya Oktoba na kulipa kodi kulingana na taarifa ya mapato

Jumatano, 7  Desemba

Tarehe ya kulipa Kodi ya Mapato ya Mshahara, Kodi ya Kuendeleza Ujuzi na kodi nyingine za zuio chini ya Kodi ya Mapato

Jumanne,20  Desemba

Tarehe ya kuwasilisha Taarifa ya VAT ya Novemba na kulipa kodi kulingana na taarifa ya mapato

Jumamosi, 31 Desemba

Walipa kodi kwa awamu:

Tarehe ya malipo ya awamu ya nne ya makadirio ya kodi kwa mwaka wa mapato wa 2022  kwa walipa kodi ambao kipindi cha malipo kinaishia Desemba 2022.

Tarehe ya malipo ya awamu ya kwanza ya makadirio ya kodi kwa mwaka wa mapato wa 2023 ambao kipindi cha malipo kinaishia Septemba  2023.

 Tarehe ya malipo ya awamu ya pili ya makadirio ya kodi kwa mwaka wa mapato wa 2023  kwa walipa kodi ambao kipindi cha malipo kinaishia Juni 2023.

Tarehe ya malipo ya awamu ya tatu ya makadirio ya kodi kwa mwaka wa mapato wa 2023  kwa walipa kodi ambao kipindi chao cha kulipa kodi kinaishia  Machi 2023.

Jumamosi, 31  Desemba

Taarifa za mwisho za mapato na malipo ya kodi ya kujikadiria mwenyewe

Tarehe ya kuwasilisha taarifa za mwisho kwa mwaka wa mapato wa 2021 kwa walipa kodi ambao kipindi chao cha kulipia kodi kinaishia Juni 2020.

Januari - Desemba

Lipia ada ya leseni ya udereva wakati unapofika