Tarehe Zipi ni Muafaka Kulipa Ushuru na Kodi?
Kodi za Mapato
- Kodi za zuio zinalipwa ndani ya siku 7 baada ya mwisho wa mwezi wa kalenda.
- Kodi zinazolipwa kwa awamu (kodi zinazokadiriwa kwa awamu) zinazilipwa katika kila robo mwaka; kwa mfano walipakodi ambao vipindi vyao vya kulipa vinaisha tarehe 30/ Desemba; awamu za malipo zitafikia wakati wa kulipwa mwishoni mwa Machi, Juni, Septemba na Desemba.
- Kodi ya kujikadiria italipwa tarehe ya mwisho ya taarifa ya mapato (miezi sita baada ya mwaka wa mapato)
- Kodi ya Kujikadiria Dharura inalipwa katika tarehe iliyobainishwa katika taarifa ya makadirio.
- Kodi Iliyorekebishwa inalipwa ndani ya siku 30 tangu tarehe ya makadirio.
Kodi ya Ongezeko la Thamani
Kodi ya Ongezeko la Thamani inalipwa ndani ya siku 20 kufuatia mwezi wa biashara yaani tarehe ya kuwailisha taarifa za kodi.
Kodi za Forodha
Ushuru na Kodi ya kuingiza bidhaa unalipwa ndani ya siku 30 tangu tarehe ya makadirio ya kodi.