Kimsingi, kuna ngazi tatu ambapo mlipakodi anaweza kukata rufaa ikiwa hajaridhishwa na maamuzi ya Kamishna Mkuu.

Rufaa kwenda katika Bodi:

Sheria inaeleza kuwa, mtu yeyote ambaye hajaridhishwa na uamuzi wa mwisho wa makadirio yaliyofanywa na Kamishana Mkuu anaweza kukata rufaa kwenye bodi. Bodi itapokea rufaa kwa kuzingatia vigezo vifuatavyo:

1   Notisi ya rufaa itolewe ndani ya siku 30 tangu Kamishna Mkuu atoe uamuzi wake wa mwisho wa makadirio ya kodi kwa mkata rufaa; na

2)     Rufaa iwasilishwe kwenye Bodi ya rufaa ndani ya siku 45 tangu tarehe ambayo taarifa ya uamuzi wa mwisho ya makadirio ya kodi ulipotolewa kwa mkata rufaa;

3)    Taarifa hiyo itoe maelezo yote kuhusu makadirio ya kodi na mawasiliano zaidi yaliyofanyika kati ya Kamishna Mkuu na mlipakodi.

 

Kukata Rufaa katika Baraza la Kodi

Baada ya uamuzi wa Bodi kufanyika, mlipakodi anaweza kuona kuwa bado hajaridhishwa na uamuzi huo. Mlipakodi ambaye hajaridhishwa na uamuzi wa bodi anaweza kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo kwenye Baraza la kodi. Rufaa kwenye Baraza la kodi itazingatia yafuatayo:

1)  Rufaa ikatwe ndani ya siku 30 tangu tarehe ya kufanyika uamuzi wa Bodi na mkata rufaa atapeleka taarifa kwa upande pinzani ndani ya siku 15 tangu siku ambayo taarifa ya rufaa iliwasilishwa mahakamani.

2)   Bodi au mahakama inaweza kurefusha ukomo wa muda uliowekwa kwa mujibu wa sheria kama imeridhishwa kuwa kushindwa kwa upande huo kutoa taarifa ya rufaa, kupinga rufaa au kutoa taarifa kwa upande pinzani kulitokana za sababu zifuatazo:

 

Rufaa katika Mahakama ya Rufaa

Mtu yeyote ambaye hajaridhishwa na uamuzi wa mahakama anaweza kuamua kukata rufaa katika mahakama ya rufaa.

Pale ambapo Mtoa pingamizi anaamua kukata rufaa katika Bodi au Mahakama kodi yoyote inayotakiwa kulipwa kwa mujibu wa sheria  itaendelea kulipwa  wakati Kamishna Mkuu akisubiri uamuzi wa mwisho  wa rufaa.