Ukurasa huu unatoa mwongozo na misimbo ambayo itakusaidia katika kulipa kwa usahihi kodi inayotakiwa. Ukurasa unatoa misimbo inayotumika kufanya malipo kwa kuonesha aina mahususi za kodi, fomu zinazotumika katika benki mahususi na malipo yanayofanyika kupitia simu za mkononi.

1.    Msimbo wa  Takwimu za Fedha za Serikali (GFS)

Hii ni namba maalumu inayotumiwa na walipakodi wakati wa malipo kwa kujaza katika hati ya malipo ya benki. 

 2.    Mfumo wa Malipo kati ya Benki moja na nyingine (TISS)

Mfumo wa Malipo kati ya Benki moja na nyingine ni njia rahisi inayotumiwa na walipakodi kuziagiza benki za biashara kuhamisha malipo kwenda Benki Kuu ya Tanzania na maudhui yaliyomo katika TISS ni: Jina la mwenye akaunti, namba ya akaunti, Jina la Benki ya Biashara, Kiasi kwa ShT, Kiasi cha pesa kwa maneno na tarehe husika.

3.   Malipo Kupitia Simu na Njia Nyingine

Huu ni mfumo ambapo walipakodi wanalipa kodi kwa njia ya simu kama M-pesa, TigoPesa, Airtel Money na Max Malipo.

Ili kufanikisha lengo la kutumia njia hii walipakodi wanashauriwa kutimiza masharti yafuatayo:

  1. Mlipakodi anapaswa kuwa mteja na amesajiliwa. Walipakodi wanashauriwa kuwasiliana na mawakala wateule waliosambaa nchi nzima.
  2.  Baada ya kusajiliwa mlipakodi atatakiwa kuingiza fedha katika akaunti ya wakala wake.

 Baada ya kutimiza masharti ya kulipa kodi kupitia mifumo iliyotolewa walipakodi wanashauriwa kufuata maelekezo yanayotolewa na mtoa huduma.

Kodi ambazo zinaweza kulipwa kupitia simu zinajumuisha kodi ya mapato binafsi, kodi kwa wafanyabiashara wadogo, kodi ya vyombo vya moto na ada.

 

Malipo ya Kodi kwa njia ya Kawaida

Ufuatao ni utaratibu ambao WalipaKodi wanahitajika kuzifuata wakati wanafanya malipo ya Kodi

1. Kutembelea ofisi ya TRA au Kituo kilichokaribu

2. Kupata makadirio ya kodi/tozo pamoja na namba ya udhibiti

3. Kuchukua taarifa ya malipo na stakabadhi ya kuwekea fedha na kujaza taarifa zinazostahili (Jina la MlipaKodi,Aina ya kodi,Namba ya Utambulisho wa    Mlipakodi,Msimbo wa      namba wa Takwimu za Fehda za Serikali,Kiasi cha kodi kinachotakiwa kulipa,tarehe ya malipo na saini ya mtu anayefanya malipo.

4. Kuiwasilisha Benki /Mpokea Fedha na kufanya malipo.

5. Kuchukua nakala ya notisi ya Benki ya malipo ya kuwekea fedha kwa ajili ya kumbukumbu.

6. Taratibu za kulipia kodi za majengo  

7.  Benki zilizoidhinishwa kupokea malipo ya Kodi