Kujaza tarakimu katika taarifa ya mapato

Usiweke senti katika tarakimu- fanya kadirio la chini kwenye tarakimu za mapato na kadirio la juu la shilingi ya karibu kwenye punguzo na makato ya kodi

Kuwasilisha taarifa ya mapato

Usichelewe kuwasilisha taarifa ya mapato TRA, hata kama hutakuwa na taarifa zote unazozihitaji. Ikiwa kuna taarifa zinazokosekana, kadiria kiwango na kuonesha ni taarifa zipi zilizokadiriwa wakati wa ujazaji wa taarifa ambazo zinahitaji kuthibitishwa.