• Zina tunza kumbukumbu za Fedha ambazo haziwezi kufutwa kwa mkono, kemikali au sumaku ya kielektroniki;
  • Zinajiendesha zenyewe na kutoa ripoti ya mauzo “Z” kila baada ya saa 24;
  • Zinatuma taarifa za kodi moja kwa moja kwenye mfumo wa TRA;
  • Zina mfumo wa tarehe usioweza kubadilishwa
  • Zinatoa risiti/ankara za kodi za kipekee;
  • Zinaweza kutumika zenyewe bila kuunganishwa kwenye mtandao;
  • Zina kifaa cha kuhifadhi umeme angalau kwa saa 48, na zinaweza kutumia betri kutoka nje katika maeneo yasiyokuwa na umeme;
  • Zinahifadhi data na kumbukumbu zilizowekwa kwenye kumbukumbu za kudumu za fedha moja kwa moja
  • Zina uwezo wa kumbukumbu za kodi ambao unahifadhi data kwa takribani miaka 5 au miamala ya siku 1800
  • Huepusha migogoro wakati wa ukaguzi na makadirio ya kodi.
  • Hurahisisha pingamizi na ukataji wa rufaa za kodi