Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inawataarifu wafanyabiashara wote kuwa imeanza zoezi la kukakugua taarifa za wafanyabiashara wote nchini ili kuhakiki taarifa zao za biashara na kama wanatunza kumbukumbu za biashara zao.  Zoezi hili litafanywa na maofisa wa TRA ambao watapita  sehemu za biashara kufanya ukaguzi

Wafanyabiashara wanaombwa kutoa ushirikiano ili kukamilisha zoezi hili kwa kuhakikisha eneo la biashara linakuwa na mtu ambaye anaweza kujibu maswali ya maafisa wa TRA pamoja na kuwa na taarifa zote za kodi. 

Tunaomba ushirikiano wenu ili kufanikisha zoezi hili.

Kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana na kituo cha huduma kwa wateja kwa simu namba 

08000780078, 0800750075, 0713800333