“Kuongeza mapato kwenye uwiano wa GDP hadi kufikia 19.9% ifikapo mwaka 2018”.

Katika utekelezaji wa sera ya serikali ya kuongeza mchango na uzalishaji wa mapato ya ndani kwa wastani wa nchi zilizo kusini mwa jangwa la Sahara, kwa kipindi cha miaka mitano ijayo TRA inakusudia kuongeza zaidi mapato hadi kufikia 19.9%. Hili litafikiwa kwa kuboresha ufanisi katika usimamizi wa kodi na kupanua wigo wa kodi kwa lengo la kukusanya mapato zaidi hususani kutoka katika sekta maalumu za migodi, mafuta na gesi, mawasiliano ya simu, utalii, ujenzi, mashamba, sekta ya fedha, watu binafsi wenye kipato cha juu, na mapato kutoka sekta zisizo rasmi.