Makosa kwa kushindwa kutumia mashine za kieletroniki

Mtu yeyote

  • Atakayeshindwa kumilki na kutumia mashine ya kieletroniki punde biashara itakapokuwa imeanza au kipindi ambacho kimewekwa na Kamishna kitakapokuwa kimeisha .
  • Kushindwa kutoa risiti au Ankara ya kieltroniki punde atakapokuwa amepokea malipoya mauzo ya bidhaa au huduma
  • Atakayetoa risiti ya kieletroniki au Ankara ya kieletroniki ambazo si za ukweli au isiyo sahihi kwa namna yoyote ile
  • Kutumia mashine za kieletroniki kwa njia ambayo inapotosha mfumo au Kamishna
  • Kusababisha au kupelekea mashine ya kieletroniki kutofanya kazi kikamilifu au kwa njia ambayo haitatoa nyaraka ya ukweli au sahihi

 Atakuwa ametenda kosa na atawajibika punde atakapopatikana na kosa kwa kulipa faini isiyopungua pointi za sarafu 200 na isiyopungua pointi za sarafu 300 au kifungo kisichozidi miaka mitatu au vyote pamoja.

 Makosa haya hayatamhusu mtu ambaye kwa mujibu wa sheria amesamehewa kumilkiau kutumia mashine za kieletroniki.

 Pale ambapo kiasi chochote cha kodi kitakuwa kimekwepwa kutokana na kosa lolote;mtu aliyehusika  atakapokuwa amebainika kwa nyongeza atalipa faini mara mbili ya kiasi ambacho kimekwepwa au kifungo kisichopungua miaka mitatu.

 Mtu ambaye atashindwa kudai risiti ya kieletroniki au kushindwa kutoa taarifa ya kutoa risiti ya kieletroniki au Ankara ya kieletroniki punde atakuwa amefanya malipo  ya bidhaa au huduma atakuwa amefanya kosa na ikithibitika atalipa faini isiyopungua pointi za sarafu 2 au isiyopungua pointi za sarafu 100.