Mamlaka ya Mapato Tanzania itakuwa na matengenezo ya mifumo ya TEHEMA (ICT System) kwa siku ya Jumapili tarehe 14Februari 2016

Mamlaka ya Mapato Tanzania inawataarifu kwamba itakuwa na matengenezo ya mifumo ya TEHAMA (ICT system) siku ya Jumapili tarehe 14 Februari 2016. Matengenezo haya yamelenga kuboresha mifumo ili kutoa huduma madhubuti.

Kipindi cha kuanza matengenezo: Jumapili tarehe 14 Februari 2016 saa 03:00 Asubuhi

Kipindi cha mwisho cha matengenezo: Jumapili tarehe 14 Februari 2016 saa 07: 00 Mchana

Matengenezo haya ni kwa mifumo yote ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwahiyo huduma za kimtandao hazitapatikana katika kipindi hiki cha matengenezo.

Kwa maswali, tafadhali wasiliana na Kituo cha Huduma kwa mteja kwa namba 0800750075/0800780078/0713800333 kwa saa za kazi, au piga namba 0786899900 kwa saa ambao si za kazi.

Mamlaka ya Mapato Tanzania inaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza kutokana na zoezi hili.