Mamlaka ya Mapato Tanzania imetoa kalenda hii ili kuwakumbusha walipakodi na wadau tarehe muhimu za kujaza taarifa za malipo ya kodi, kufanya malipo ya kodi na matukio mengine muhimu. Kalenda hii itawasaidia katika kupanga masuala yenu ya kodi.
Tarehe |
Suala/Tukio |
Ijumaa,7 Januari |
Tarehe ya kulipa Kodi ya Mshahara, Kodi ya Kuendeleza Ujuzi na kodi nyingine za zuio chini ya Kodi ya Mapato |
Alhamisi, 20 Januari |
Tarehe ya kuwasilisha Ripoti za VAT za Desemba 2020 na kulipa kodi kulingana na ripoti |
Jumatano, 26 Januari |
Siku ya Forodha Duniani |
Jumatatu, 7 Februari |
Tarehe ya kulipa Kodi ya Mshahara, Kodi ya Kuendeleza Ujuzi na kodi nyingine za zuio chini ya Kodi ya Mapato |
Jumatatu, 21 Februari |
Tarehe ya kuwasilisha Ripoti ya VAT na kulipa kodi kulingana na ripoti |
Jumatatu, 7 Machi |
Tarehe ya kulipa Kodi ya Mshahara, Kodi ya Kuendeleza Ujuzi na kodi nyingine za zuio chini ya Kodi ya Mapato |
Jumatatu,21 Machi |
Tarehe ya kuwasilisha Ripoti ya VAT ya Februari na kulipa kodi kulingana na ripoti ya kodi |
Alhamisi, 31 Machi |
Walipakodi ya Mapato kwa Awamu: Tarehe ya malipo ya awamu ya kwanza ya makadirio ya kodi kwa mwaka wa mapato wa 2022 kwa walipakodi ambao kipindi cha hesabu kinaishia Desemba 2022 Tarehe ya malipo ya awamu ya nne ya makadirio ya kodi kwa mwaka wa mapato wa 2021 kwa walipakodi ambao kipindi cha malipo ya kodi kinaishia Machi 2022 Tarehe ya malipo ya awamu ya tatu ya makadirio ya kodi kwa mwaka wa mapato wa 2022 kwa walipakodi ambao kipindi cha malipo ya kodi kinaishia Juni 2022 Tarehe ya malipo ya awamu ya pili ya makadirio ya kodi kwa mwaka wa mapato wa 2021 kwa walipakodi ambao kipindi cha malipo ya kodi kinaishia Septemba 2022 |
Alhamisi,31 Machi |
Ripoti ya mwisho ya mapato na malipo ya makadirio binafsi ya kodi Tarehe ya kuwasilisha ripoti ya mwisho ya mapato kwa mwaka wa mapato wa kwa walipakodi ambao kipindi cha kulipa kodi 2020 kinaishia Septemba 2021 |
Alhamisi,7 Aprili |
Tarehe ya kulipa Kodi ya Mshahara, Kodi ya Kuendeleza Ujuzi na kodi nyingine za zuio chini ya Kodi ya Mapato |
Jumatano,20 Aprili |
Tarehe ya kuwasilisha Taarifa za VAT za Machi na kulipa kodi kulingana na ripoti |
Jumamosi, 7 Mei |
Tarehe ya kulipa Kodi ya Mshahara, Kodi ya Kuendeleza Ujuzi na kodi nyingine za zuio chini ya Kodi ya Mapato |
Ijumaa, 20 Mei |
Tarehe ya kuwasilisha Taarifa za VAT za Aprili na kulipa kodi kulingana na taarifa za kodi |
Jumanne, 7 Juni |
Tarehe ya kulipa Kodi ya Mshahara, Kodi ya Kuendeleza Ujuzi na kodi nyingine za zuio chini ya Kodi ya Mapato |
Jumatatu,20 Juni |
Tarehe ya kuwasilisha taarifa ya VAT ya mwezi Mei na kulipa kodi kulingana na taarifa ya mapato |
Jumapili,26 Juni |
Siku ya madawa haramu Duniani |
Alhamisi,30 Juni |
Walipakodi kwa awamu: Tarehe ya malipo ya awamu ya pili ya makadirio ya kodi kwa mwaka wa mapato 2022 kwa walipa kodi ambao kipindi chao cha malipo ya kodi kinaishia Desemba 2022 Tarehe ya malipo ya awamu ya tatu ya makadirio ya kodi kwa mwaka wa mapato wa 2022 kwa walipa kodi ambao kipindi cha malipo ya kodi kinaishia Septemba 2022. Tarehe ya malipo ya awamu ya nne ya makadirio ya kodi kwa mwaka wa mapato wa 2022 kwa walipa kodi ambao kipindi cha malipo ya kodi kinaishia Juni 2022. Tarehe ya malipo ya awamu ya kwanza ya makadirio ya kodi kwa mwaka wa mapato wa 2023 kwa walipa kodi ambao kipindi cha malipo ya kodi kinaishia Machi 2023. |
Alhamisi, 30 Juni |
Taarifa ya mwisho ya mapato na malipo ya makadirio binafsi ya kodi Tarehe ya kuwasilisha taarifa ya mwisho ya mapato kwa mwaka 2021 kwa walipa kodi ambao kipindi cha malipo ya kodi kinaishia Desemba 2021. |
|
|
Alhamisi, 7 Julai |
Tarehe ya kulipa Kodi ya Mapato ya Mshahara, Kodi ya Kuendeleza Ujuzi na kodi nyingine za zuio chini ya Kodi ya Mapato |
Jumatano, 20 Julai |
Tarehe ya kuwasilisha Taarifa za VAT na kulipa kodi kulingana na taarifa za mapato |
Jumapili, 7 Agosti |
Tarehe ya kulipa Kodi ya Mapato ya Mshahara, Kodi ya Kuendeleza Ujuzi na kodi nyingine za zuio chini ya Kodi ya Mapato |
Jumatatu, 22 Agosti |
Tarehe ya kuwasilisha Taarifa za VAT za Julai na kulipa kodi kulingana na taarifa ya mapato |
Jumatano, 7 Septemba |
Tarehe ya kulipa Kodi ya Mapato ya Mshahara, Kodi ya Kuendeleza Ujuzi na kodi nyingine za zuio chini ya Kodi ya Mapato |
Jumanne,20 Septemba |
Tarehe ya kuwasilisha Taarifa za VAT za Agosti na kulipa kodi kulingana na taarifa za mapato |
Ijumaa, 30 Septemba |
Walipakodi kwa awamu: Tarehe ya malipo ya awamu ya tatu ya makadirio ya kodi kwa mwaka wa mapato wa 2022 kwa walipakodi ambao kipindi cha malipo ya kodi kinaishia Desemba 2022. Tarehe ya malipo ya awamu ya nne ya makadirio ya kodi kwa mwaka wa mapato wa 2022 kwa walipakodi ambao kipindi cha malipo ya kodi kinaishia Septemba 2022. Tarehe ya malipo ya awamu ya kwanza ya makadirio ya kodi kwa mwaka wa mapato wa 2023 kwa walipakodi ambao kipindi chao cha kulipa kodi kinaishia Juni 2023. Tarehe ya malipo ya awamu ya pili ya makadirio ya kodi kwa mwaka wa mapato wa 2023 kwa walipakodi ambao kipindi cha kulipa kodi kinaishia Machi 2023. |
Ijumaa, 30 Septemba |
Ripoti ya mwisho ya mapato na malipo ya kodi za kujikadiria Tarehe ya kuwasilisha ripoti ya mwisho ya kodi kwa mwaka wa mapato wa 2021 kwa walipakodi ambao kipindi cha malipo ya kodi kinaishia Machi 2022. |
Ijumaa, 7 Oktoba |
Tarehe ya kulipa Kodi ya Mapato ya Mshahara, Kodi ya Kuendeleza Ujuzi na kodi nyingine za zuio chini ya Kodi ya Mapato |
Alhamisi, 20 Oktoba |
Tarehe ya kuwasilisha Taarifa ya VAT ya Septemba na kulipa kodi kulingana na taarifa ya mapato |
Jumatatu, 7 Novemba |
Tarehe ya kulipa Kodi ya Mapato ya Mshahara, Kodi ya Kuendeleza Ujuzi na kodi nyingine za zuio chini ya Kodi ya Mapato |
Jumatatu,21 Novemba |
Tarehe ya kuwasilisha Taarifa ya VAT ya Oktoba na kulipa kodi kulingana na taarifa ya mapato |
Jumatano, 7 Desemba |
Tarehe ya kulipa Kodi ya Mapato ya Mshahara, Kodi ya Kuendeleza Ujuzi na kodi nyingine za zuio chini ya Kodi ya Mapato |
Jumanne,20 Desemba |
Tarehe ya kuwasilisha Taarifa ya VAT ya Novemba na kulipa kodi kulingana na taarifa ya mapato |
Jumamosi, 31 Desemba |
Walipa kodi kwa awamu: Tarehe ya malipo ya awamu ya nne ya makadirio ya kodi kwa mwaka wa mapato wa 2022 kwa walipa kodi ambao kipindi cha malipo kinaishia Desemba 2022. Tarehe ya malipo ya awamu ya kwanza ya makadirio ya kodi kwa mwaka wa mapato wa 2023 ambao kipindi cha malipo kinaishia Septemba 2023. Tarehe ya malipo ya awamu ya pili ya makadirio ya kodi kwa mwaka wa mapato wa 2023 kwa walipa kodi ambao kipindi cha malipo kinaishia Juni 2023. Tarehe ya malipo ya awamu ya tatu ya makadirio ya kodi kwa mwaka wa mapato wa 2023 kwa walipa kodi ambao kipindi chao cha kulipa kodi kinaishia Machi 2023. |
Jumamosi, 31 Desemba |
Taarifa za mwisho za mapato na malipo ya kodi ya kujikadiria mwenyewe Tarehe ya kuwasilisha taarifa za mwisho kwa mwaka wa mapato wa 2021 kwa walipa kodi ambao kipindi chao cha kulipia kodi kinaishia Juni 2020. |
Januari - Desemba |
Lipia ada ya leseni ya udereva wakati unapofika |