Uwasilishaji wa Taarifa (Ritani) ya Mwisho ya Mapato

Mlipakodi anaepaswa kutunza anatakiwa kuwasilisha taarifa ya mwisho ya mapato  ndani ya miezi sita tangu tarehe ya kufunga hesabu za mwaka wa mapato. Taarifa hii itaambatishwa na hesabu za mizania za mwenendo wa biashara husika. Ikumbukwe kuwa taarifa hii sio lazima kwa mlipakodi alie chini ya mfumo wa makisio, labda kama ameamua kutunza kumbukumbu za biashara yake.


Mtu binafsi anapaswa kujaza taarifa ya mwisho ya mapato kwenda kwa Kamishna katika kipindi kisichozidi miezi sita baada ya kila mwisho wa mwaka wa mapato.

Kamishna anaweza kuongeza muda wa kujaza taarifa ya mapato kufuatia maombi ya mwombaji kwa maandishi na kwa kuzingatia kanuni na taratibu ambazo Kamishna ataona zinafaa.

Chini ya mfumo wa makisio mtu binafsi halazimiki kujaza fomu yoyote ya taarifa ya mapato badala yake anaweza akalipa kwa awamu kama kiwango kilichokadiriwa kinazidi SHT 50,000 kwa mwaka.