Print

 Fomu za taarifa ya mapato zina kurasa saba na kurasa za nyongeza kwa ajili ukokotozi wa aina zifuatazo za mapato na faida:

i.        Faida inayotokana na mauzo ya hisa na amana katika mashirika

ii.        Faida inayotokana na mauzo ya rasilimali isipokuwa hisa, amana au bidhaa za kibiashara.

iii.        mapato ya marejesho kwa kampuni binafsi za kudumu za ndani

iv.        Mapato yatokanayo na bima ya jumla

v.        Mapato yatokanayo na biashara ya bima ya maisha

vi.        Mapato yatokanayo na shughuli za uchimbaji wa madini.