Taarifa ya mapato inakutaka kubainisha mapato yako yatakayotozwa kodi: Hii inahusisha:unapaswa kupitia kurasa za taarifa za fedha za biashara au uwekezaji zilizotumwa pamoja na taarifa ya mapato ili kuhakikisha kwamba kurasa zote zinazotakiwa kwa ajili ya aina mbalimbali za biashara au mapato na faida za uwekezaji zimepokelewa. Kama kuna kurasa zozote zinakosekana au unahitaji kurasa za ziada unatakiwa kuwasiliana na ofisi ya TRA iliyo karibu au kupitia  Kituo cha mawasiliano

                    i.        jumla ya mapato yako.

                   ii.        marejesho yoyote ya mapato kutoka katika vyanzo vya kudumu vya mapato ya ndani.

                  iii.        kama hukuwa mkazi wakati wa mwaka wa mapato na kwamba kodi ililipwa kwa zuio na awamu ambapo kulikuwa na mkopo wa kodi kwenye mwaka wa mapato.

Taarifa zilizojazwa zinaweza kuchunguzwa ili kuhakikisha kuwa ni sahihi na adhabu itatolewa kwa atakayetoa taarifa za uongo au kutokuweka mapato. Ikiwa utahitaji msaada wakati wa kujaza taarifa zako, wasiliana na ofisi ya TRA iliyo karibu  au kupitia Kituo cha mawasiliano

Ikiwa utahitaji kuongeza muda baada ya muda uliowekwa kujaza taarifa za mapato, utatakiwa kutuma maombi ili kupata idhini ya Kamishna kabla ya muda uliowekwa kisheria kupita.

Baada ya kukamilisha ujazaji wa taarifa yako ya mapato, hakikisha kwamba umejaza taarifa zote zinazohitajika. Ukishakamilisha kujaza, weka saini na tarehe katika tamko lako kisha tuma fomu iliyokamilika TRA. Tuma fomu ikiwa na tarehe ya uthibitisho kwenda TRA. Tuma fomu ikiwa na uthibitisho wa ukokotozi, kurasa za ziada na hesabu zilizokaguliwa (taarifa za fedha). Litakuwa jambo jema kutunza nakala ya fomu iliyojazwa kwa ajili ya kumbukumbu zako.