1.0 UTANGULIZI

Kwa zaidi ya miaka 17 Mamlaka ya Mapato Tanzania imekua kutoka kwenye usimamizi wa kodi ambao unatoa huduma za kodi kwa ajili ya kukusanya mapato hadi shirika madhubuti ambalo linatoa huduma zote sehemu moja kwa aina zote za kodi ambazo zinaongoza katika utoaji wa huduma katika kiwango cha ISO 9000:2008 cha uthibitisho wa shirika.

Mpango wa nne wa shirika umefikiriwa kwenye mabadiliko katika mazingira ya uendeshaji wa TRA ambayo yanajumuisha  kiwango cha ustaarabu wa wadau, haja ya kutoa huduma ambazo zinafikia au kuzidi matarajio ya wateja na haja ya serikali kujitegemea kwa kuongeza ukusanyaji wa mapato ya ndani ili kupunguza utegemezi wa misaada katika Bajeti ya Serikali.

Mpango umeandaliwa kwa kutumia masuala manne yanayokamilishana ambayo ni ya kifedha, wateja, michakato ya ndani na ujifunzaji na ubunifu ambapo malengo mkakati yamefungamana kukiwa na uhusiano wa sababu na athari. Mitazamo na malengo mkakati yake  imewekwa katika makundi katika malengo mkakati ya urahisi , ukubalifu na uboreshaji endelevu  ili kujenga fikra mkakati za TRA  kwa miaka mitano ijayo.