Katika kutambua masharti ya mwongozo yaliyotajwa hapo juu, ni wazi kwamba wakati wa utekelezaji wa mpango wa nne wa shirika, utegemezi mkubwa wa kodi ya ndani unadhihirisha upunguzaji wa utegemezi wa kodi za biashara za kimataifa.  Ufanisi katika usimamizi wa kodi ni eneo lingine la kumakinikiwa kuhakikisha thamani ya pesa katika uendeshaji kwa kutumia kiwango cha juu ya teknolojia ambayo itawezesha huduma ya kulipa kodi kielektroniki katika usajili, kujaza fomu, malipo na mawasiliano ya jumla ya kieletroniki na TRA. Njia hii mpya ya kufanya shughuli inahitaji madadiliko kwa walipa kodi na usimamizi wa kodi kwa lengo la kutumia mbinu na mkabala mpya. Shirika linaingia katika kipindi kipya kinachosisitiza katika urahisi wa walipakodi katika kuwasiliana na TRA, na kuongeza ukubalifu na kuendelea kutumia mbinu bora katika usimamizi wa kodi  kupitia uboreshaji endelevu ili kutambua madhumuni ya Mpango wa nne wa Shirika. Mada Mkakati kwa mpango wa nne wa shirika ni urahisi, ukubalifu na uboreshaji endelevu.

 

 MALENGO MKAKATI

Mada zilizobainishwa zinaweza kufanikiwa ikiwa tu zitakuwa na malengo mkakati sambamba na mitazamo linganifu minne. Uhusiano wa sababu na athari unatoa uwiano katika matokeo halisi (kifedha na mteja) na sababu dhahania za utendaji (michakato, watu, teknolojia na ujuzi). Malengo mkakati, hatua na shabaha vinawakilisha  mambo yanayohitajika kukamilishwa na shirika. Malengo mkakati kumi na mawili yaliyoainishwa katika masuala manne yamefafanuliwa katika jedwali hapa chini.

 

Suala

Malengo Mkakati

Fedha

 1. Kuboresha ufanisi wa uendeshaji
 2. Kuongeza mchango wa mapato ya ndani

Mteja

 1. Kuwa mbia mwepesi kushawishi, na mwenye uwezo wa kutumia teknolojia

Mchakato

 1. Kurahisisha Usajili, tathmini na malipo ili kuongeza huduma binafsi.
 2. Kuhamasisha ulipaji wa haraka ili kuboresha uwezeshaji wa kibiashara
 3. Kuwezesha uboreshaji wa utawala na sera
 4. Kuwa na ufanisi katika kukusanya na kuhesabu, ukaguzi na uchunguzi na vipingamizi.
 5. Kukuza elimu na huduma inayolenga katika sehemu mahususi ili kuwezesha makubaliano ya hiari.

 

Kujifunza & ubunifu

1. Kuboresha uwezo wa kimkakati wa rasilimali watu.

 1. Kujenga utamaduni unaoongeza utendaji, ubunifu, ushirikiano na uongozi.
 2. Kuongeza upatikanaji na usambazaji wa  TEHAMA
 3. Kuongeza uwezo wa utawala bora

 

 

  

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

  

 

Kanzi ya Ufuatiliaji na Tathmini TRA

Kanzi ya TRA ya Ufuatiliaji na Tathmini itaendelea kutumika kama zana ya utaratibu wa ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa Mpango wa Shirika. Kila idara inapaswa kuweka hali yao ya utekelezaji katika Kanzi ya TRA kila mwezi.  Wakati ufuatiliaji ni mchakato endelevu, tathmini zitafanywa mara moja kwa kila robo mwaka na ripoti zitaandaliwa kwa ajili ya menejimenti, Bodi na Wadau wengine. Kanzi ni mfumo mmoja wa kutoa ripoti ya utekelezaji wa Mpango wa Shirika kisha taarifa/data zilizowekwa katika mfumo huu lazima zithibitishwe na Wakuu wa Idara wanaohusika kama zilivyowekwa katika Kanzi.

Maadili ya msingi

Uwajibikaji:  Tunajenga na kuendeleza shirika linalojali na kuendeleza uwajibikaji

Uadilifu:  Tunaamini katika kutenda haki na uaminifu kwa walipakodi na wadau wengine katika shughuli zetu zote.

Weledi: Tunawajibika kufuata sheria kikamilifu, kwa uaminifu na kuaminika kwa kutumia ujuzi na elimu kama mhimili katika kusimamia mahitaji yetu.