Ada ya mwaka ya leseni ya chombo cha moto inatozwa wakati wa usajili wa kwanza wa chombo cha moto na kila mwaka baada ya hapo. Ada ya mwaka inategemea ukubwa wa injini kama inavyooneshwa katika jedwali hapa chini:

 

Transfer fees

Ada za kubadili mmiliki

Motor vehicle

Gari

TSHS 50,000

Motor cycle

Pikipiki

TSHS 27,000

New registration card on transfer

Kadi mpya ya usajili kutokana na kubadili mmiliki

TSHS

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Hata hivyo, matrekta, pikipiki na pikipiki za magurudumu matatu (bajaji) zimeondolewa katika malipo ya ada ya mwaka ya leseni za vyombo vya moto lakini yanapaswa kulipa ada ya ukaguzi wa vifaa vya zimamoto ambayo ni shilingi 10,000.

 

Malipo ya ada ya mwaka ya leseni za vyombo vya moto yanapaswa kufanyika kupitia simu za viganjani, mawakala wa Maxmalipo au kupitia benki zilizoidhinishwa.

 

Namna ya kujisajili kwa ajili ya malipo:-

 

  • Ukadiriaji: Tuma ujumbe wa simu wenye neno ''kadiria'', acha nafasi na ingiza namba ya usajili ya chombo cha moto mf. KADIRIA T765AAU kisha tuma kwenda 15341. Utapokea ujumbe wa kiasi cha kodi unachotakiwa kulipa.
  • Malipo: Tuma neno ''Sajili'' acha nafasi, ingiza namba ya usajili ya chombo cha moto mf. SAJILI T765AAU kisha tuma kwenda 15341 kupata namba ya kumbukumbu.
  • Tumia namba ya kumbukumbu uliyopewa kulipia kwa njia ya simu (yaani M-Pesa, Tigopesa au Airtelmoney) madawati ya benki ya CRDB au mawakala wa MaxMalipo.
  • Namba ya kampuni kwa TIGO-PESA na M-PESA ni 800600. Kwa Airtel-Money ni TRAMAGARI.
  • Uchukuaji wa stika ya leseni ya mwaka ya chombo cha moto: tumia namba ya kumbukumbu uliyopewa kupitia ujumbe wa simu na kitambulisho kuchukua stika yako kwenye ofisi yoyote ya TRA.

 

Angalizo: Mtu mwingine yeyote haruhusiwi kukuchukulia stika.