Habari & Matukio
TRA MOROGORO YATOA ELIMU YA KODI KWA KLABU ZA KODI KATIKA SHULE ZA SEKONDARI WILAYANI KILOSA
09 May, 2026
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Morogoro, tarehe 07/05/2026 ilitoa elimu ya kodi kwa wanafunzi wa Klabu za Kodi zilizopo Wilayani Kilosa.
Afisa wa Kodi Bw. Zephania Mange, CPA Alex Mwambenja pamoja na CPA Jewel Mosha kwa kushirikiana na Bi. Immaculate Chaggu, Afisa wa Elimu kwa Mlipakodi Mkoa wa Morogoro, kwa pamoja waliweza kuwahamasisha wanafunzi kushiriki kikamilifu katika shughuli za Klabu ya Kodi ili kujifunza masuala ya kodi na kuwa mabalozi wazuri na waaminifu katika jamii, hususan kwa kudai risiti kwa kila manunuzi wanayofanya.
Aidha, zawadi zilitolewa kwa Wakuu wa Shule pamoja na Walimu walezi wa Klabu ya Kodi ili kusaidia usimamizi na uendelezaji wa shughuli za klabu hiyo shuleni.
Lengo la shughuli hiyo ni kuimarisha ushirikiano na ushiriki kati ya TRA na Klabu za Kodi shuleni sambamba na kuongeza uelewa wa masuala ya kodi kwa wanafunzi.