TRA MKOA WA IRINGA YAFUNGUA VILABU VYA KODI
28 February, 2025
Mamlaka ya Mapato Mkoa wa Iringa imezindua Klabu za Kodi Nne katika shule Nne za Sekondari ambazo ni Shule ya Sekondari ya Don Bosco Seminary, Shule ya Sekondari ya JJ Mungai, Shule ya Sekondari ya Changarawe pamoja Sekondari ya Kawawa zote zipo wilaya ya Mufindi.
Klabu hizo zimezinduliwa na Afisa Tarafa ya IFWANGI Bi Faraja Ndipo kwa niaba ya Katibu Tawala wilaya ya Mufindi. Bi Faraja amewataka wanaklabu za kodi kutumia fursa mbalimbali kutoka TRA ili wajifunze masuala ya kodi na hatimaye wawe chachu ya Elimu katika jamii.
Pia Mwakilishi wa Meneja wa TRA wilaya ya Mufindi Bw. Katikiro amewasisitiza wanaklabu wa shule hizo kuwa mabalozi wema kwa jamii kwa kushiriki moja kwa moja katika kutoa elimu juu ya umuhimu wa kulipa kodi pamoja kutimiza wajibu wa DAI RISITI ZA EFD kwa kila wanapofanya Manunuzi.
Habari Mpya
TRA KAGERA YATEMBELEA KLABU YA KODI SEKONDARI YA KISHAI
TRA YASHIRIKI MAHAFALI ZANAKI SEKONDARI