Emblem TRA Logo

MAFUNZO YA MFUMO WA USAJILI WA VYOMBO VYA MOTO (CMVRS) NA MFUMO WA USAJILI WA LESENI ZA UDEREVA (CDLS)

12 April, 2025

Featured Image

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetoa mafunzo kuhusiana na mfumo mpya wa usajili wa magari (CMVRS) na mfumo wa usajili wa leseni ya udereva (CDLS)  kwa Jumuiya mbalimbali za Kodi kwa Wanafunzi wa Vyuo mbalimbali katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Lengo ni kuwajengea uwezo wanafunzi kufahamu mifumo hii mipya ili waweze kufanya kwa vitendo na kuweza kusambaza elimu hiyo kwa jamii inayowazunguka.
Jumuiya za kodi ni wadau wakubwa katika usambazaji wa elimu katika ngazi mbalimbali kwenye jamii. Faida za mifumo hii ni kumrahisishia Mlipakodi  kufanya usajili wa magari na leseni za udereva mtandaoni na kupunguza hitaji la matumizi ya karatasi na kutembelea ofisi za TRA.