Emblem TRA Logo

Utangulizi

 

Kodi ya zuio ni kiasi cha kodi kinachozuiwa na mtu anapomlipa mtu mwingine kutokana na bidhaa zilizosambazwa au huduma iliyotolewa na mlipwaji. Mtu anayepokea au anayestahili kupokea malipo ambayo kwayo kodi ya mapato inatakiwa kuzuiwa ni mkatwaji wa kodi ilhali mtu anayepaswa kuzuia kodi ya mapato kutoka katika malipo yaliyofanyika kwa mkatwaji anajulikana kama Wakala wa kodi ya zuio.

 

Malipo yanayostahili kukatwa kodi ya zuio

Kodi ya zuio inatozwa katika malipo husika ikiwa ni pamoja na malipo yanayopaswa kujumuishwa katika kukokotoa mapato ya mwajiriwa yanayostahili kukatwa kutoka kwa mwajiriwa katika ajira, malipo ya mapato ya uwekezaji ikiwa ni pamoja na magawio, riba, malipo ya maliasili, pango au mrabaha, malipo ya huduma na malipo ya mikataba na malipo ya bidhaa zilizosambazwa serikalini na kwenye taasisi zake.

 

Taarifa na Muda wa Kulipa Kodi Iliyozuiwa

Kila wakala wa kodi ya zuio atalipa kwa Kamishna kodi ya zuio aliyozuia ndani ya siku 7 baada ya kila mwisho wa mwezi wa kalenda.

 

Hati ya Kodi ya Zuio

Hati ya kodi ya zuio inapatikana kwenye mtandao kupitia kwenye mfumo wa malipo na Mzuiaji au Mzuiwa anaweza kuipata mara malipo yanapokuwa yamefanyika.

 

Aina za Kodi za Zuio

Sheria imegawanya kodi ya zuio katika aina kuu mbili, ambazo ni: -

·         Kodi za Zuio za mwisho

·         Kodi za Zuio zisizo za Mwisho

Kodi za Zuio za Mwisho ni kodi ambazo mzuiwa hawezi kudai punguzo lolote la kodi wakati wa kukokotoa kodi ya mapato inayolipwa kwa mwaka wa mapato.

Kodi za Zuio zisizo za Mwisho: ni kodi ambazo mzuiwa anastahili punguzo la kodi kiasi sawa na kodi inayochukuliwa kuwa imelipwa kwa mwaka wa mapato ambamo kiasi hicho kimekokotolewa.

 

VIWANGO VYA KODI YA ZUIO

Chanzo cha kodi

Mkazi

Asiye mkazi

Gawio kutoka kwenye makampuni yaliyoorodheshwa kwenye soko la hisa la Dar es Salaam

5%

5%

Gawio kwa makampuni mkazi kwenda kwa kampuni mkazi yanayomiliki hisa kwa 25% au zaidi

5%

Hakuna

Gawio kutoka kwenye makampuni mengine

10%

10%

Riba

10%

10%

Mirabaha

15%

15%

Huduma za kiutawala na kiufundi (Uchimbaji Madini, Mafuta na Gesi)

1%

15%

Watoa huduma za usafirishaji (Ndege/Meli) wasio wakazi/wakodisha ndege wasio na makazi ya kudumu

Hakuna

5%

Mapato kutokana na ukodishaji wa nyumba/majengo

10%

15%

Malipo ya bima

Hakuna

10%

Wajibu wa kuzuia VAT kwa ununuaji wa bidhaa na Wakala wa Zuio chini ya Kifungu cha 5(5) cha Sheria ya VAT.

            3%

Hakuna

Wajibu wa kuzuia VAT kwa ununuaji wa huduma na Wakala wa Zuio chini ya Kifungu cha 5(5) cha Sheria ya VAT.

            6%

Hakuna

Malipo ya manunuzi ya chumvi

            2%

Hakuna

Kamisheni ya Matangazo ya michezo ya kubahatisha

           10%

Hakuna

Malipo kutokana na kukodisha chombo cha moto

           10%

Hakuna

Malipo ya mazao ya misitu

            2% ya mauzo ghafi

Hakuna

Malipo yatokanayo na maliasili

15%

15%

Ada za huduma

5%

15%

Faida ya kuuza hisa, ardhi na majengo

10%

20%

Malipo ya Wakurugenzi (wakurugenzi wasio na ajira za kudumu) 

15%

15%

Asilimia ya faida inayotolewa kwa wakala kutoka kwa watoa huduma za utumaji fedha kwa njia ya simu za mkononi.

10%

Hakuna

Mauzo yanayohusisha mauzo ya mazao ya Kilimo, mifugo na uvuvi yanapouzwa kwenye Kampuni na Mashirika yote yanayojihusisha na usindikaji na ununuzi wa mazao

2% Mauzo ghafi

Hakuna

Malipo kwa bidhaa zilizosambazwa na mtu yeyote kwa serikali na taasisi zake.

2% kabla ya kukatwa Kodi

Haihusiki

Kodi ya Pango (Kwa matumizi ya kibiashara)

10%

20%

Malipo mengine ya zuio

15%

15%

Malipo yaliyofanywa kuhusiana na ununuzi wa madini ya thamani, vito na vito vingine vya thamani vilivyotolewa na mwenye leseni ya msingi ya uchimbaji madini au mchimbaji migodi 

 2%

N/A

Malipo yaliyofanywa kwa mkazi kuhusiana na upunguzaji wa hewa ya ukaa iliyothibitishwa

   10%

N/A

Ndege

     10%

15%