Emblem TRA Logo
Uahirishaji wa Kodi ya Ongezeko la Thamani

Uahirishaji wa kodi ya ongezeko la thamani ni nini?

Uahirishaji wa kodi ya ongezeko la thamani (VAT Deferment) ni msamaha wa VAT unaotolewa kwa waingizaji na wanunuzi wa bidhaa, mitambo au vifaa vya uzalishaji mali (capital goods) vilivyoko kwenye sura ya 84, 85 na baadhi ya 90 ya Mfumo wa Ushuru wa Pamoja wa EAC (EAC CET), kwa kuahirisha malipo ya VAT juu ya bidhaa hizo baada ya kuwasilisha maombi na kupata idhini kutoka kwa Kamishna Mkuu wa TRA.

Wigo wa bidhaa zinazostahili msamaha huu pia umeongezwa kujumuisha matrekta ya barabarani na matrela (trailers) yaliyoainishwa katika vichwa vya 87.01 na 87.16, iliyotengenezwa ndani ya nchi au iliyokusanywa katika ghala la dhamana ya forodha. 

Hata hivyo kutakuwa na ukomo wa Uahirishaji wa kodi la ongezeko la thamani iatakapofika tarehe 30 Juni 2026 kutokana na kifungu cha 11(1) cha sheria ya Kodi la Ongezeko la Thamani

Masharti ya Msamaha wa VAT Deferment

a. Bidhaa zinazoingizwa lazima ziwe ni mitambo au vifaa vya uzalishaji mali isipokuwa matrekta na matrela yaliyotengenezwa hapa nchini. 

b. Mwingizaji wa bidhaa awe anafanya shughuli za kiuchumi, awe na TIN na amesajiliwa kwa ajili ya VAT. 

c. Mwingizaji awe anauza bidhaa au huduma zinazotozwa kodi ya ongezeko la thamani kwa kiwango cha angalau asilimia 90. 

d. Awe anahifadhi kumbukumbu sahihi na anawasilisha ritani za VAT kwa wakati. 

e. Awe anatekeleza wajibu wake kwa mujibu wa Sheria ya VAT na sheria nyingine za kodi. 

f. Thamani ya VAT kwa bidhaa zinazoingizwa lazima iwe angalau TZS 10,000,000/=.

 

Utaratibu wa Kuomba VAT Deferment

Mwingizaji wa bidhaa atawasilisha maombi kwa kujaza Fomu ITX 247.02.E (inajazwa mtandaoni kupitia mfumo wa TanESW) pamoja na nyaraka zifuatazo:

a. Nyaraka za uingizaji wa bidhaa (Bill of Lading, Ankara ya malipo na Packing List). 

b. Fomu ya uhamishaji wa umiliki (C16) kwa bidhaa zilizonunuliwa kutoka kwenye bondi. 

c. Cheti cha TIN. 

d. Cheti cha VRN. 

e. Ritani za VAT za miezi miwili ya hivi karibuni. 

f. Cheti cha kutolimbikiza deni la kodi (Tax Clearance Certificate). 

g. Leseni ya viwanda / biashara au cheti cha CRB (kwa wakandarasi