Utangulizi
Mtu ambaye anatarajia kuingiza bidhaa ambazo zitakaa kwa muda mfupi katika nchi wanachama ataingiza bidhaa bure baada ya kuomba na kuruhusiwa na Kamishna kwa kuzingatia bidhaa hizo zitaondoshwa tena baada ya kuisha kwa muda wake wa kukaa.
Bidhaa ambazo zinaingizwa kwa dhumuni la matumizi ya muda mfupi zinajumuisha:
a) sampuli za wasafiri za kibiashara
b) Bidhaa, ikiwemo vifaa kwa ajili ya kutengeneza jukwaa, inayoingizwa kwa ajili ya Maonesho au burudani
c) Bidhaa zinazoingizwa kwa ajili ya ukarabati na matengenezo
d) Bidhaa za uendelezaji utalii ambazo hazijapigwa marufuku
e) Magari yote na bidhaa zinazoingizwa na raia aliye chini ya COMESA au SADC au Jumuiya ya Afrika Mashariki
f) Bidahaa nyingine ambazo Kamishna ataziruhusu kuendana na vigezo atakavyo viweka.
Mtu ambaye anatarajia kuingiza bidhaa kwa muda mfupi anapaswa kufanya maombi kwa kujaza fomu namba C.17 (TANCIS) na maombi hayo yaeleze;
a) Taarifa kamili ya mzigo unaoingizwa, ueleze asili ya bidhaa na dhumuni lake, utambulisho; na
b) Makadirio ya tarehe na mahali ambapo mzigo utaondoshwa, pia mwingizaji anatakiwa kuweka kiasi ambacho kitakachotosheleza kodi ya bidhaa hiyo au awekeze dhamana katika Maghara ya Dhamana ya Forodha na afisa atathibitisha.
KUMBUKA
Afisa atapitia maombi ya mmliki, na ataeleza kiasi cha kodi ambacho kinapaswa kutozwa, na kiasi cha kuweka kama dhamana. Kama bidhaa zitakuwa za kuondoshwa katika mahali ambapo ni tofauti na mahali alipoingizia bidhaa, maombi yatafanyika katika nakala tatu. Kama Afisa atahitaji, Ankara au nyaraka ambazo zitaonesha uwalali wa thamani ya bidhaa, mwingizaji anapaswa kuambatanisha kwenye maombi yake. Magari na bidhaa zinazoingizwa zinapaswa kuondoshwa ndani ya kipindi cha miezi kumi na mbili kutokea tarehe ya kuingiza mzigo.
Habari & Matukio
TRA YAKUTANA NA UJUMBE WA SHIRIKA LA FEDHA DUNIANI - IMF