Emblem TRA Logo
Msamaha wa Ushuru wa Forodha na Bidhaa kwa Watumishi wa Umma

Afisa wa umma anayestahili msamaha ni nani?

Katika muktadha wa msamaha wa Ushuru wa Forodha na Ushuru wa Bidhaa, mtumishi wa umma anayestahili msamaha huu ni: -

  1. Mfanyakazi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali za Mitaa, au shirika la umma ambalo zaidi ya 50% ya bajeti yake inatokana na ruzuku ya Serikali.
  2. Anayeshika ngazi ya mshahara ya TGS D au juu zaidi katika Serikali Kuu, au ngazi inayolingana katika Serikali za Mitaa au mashirika ya umma.
  3. Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pia wanajumuishwa katika kundi hili.

 

Msingi wa Kisheria na Wigo wa Msamaha

Msamaha huu unahusu ushuru wa Forodha (Import Duty) na ushuru wa Bidhaa (Excise Duty) umetolewa chini ya mamlaka ya Notisi za Serikali Na. 520 na 522 za mwaka 1995.

 

Mfumo wa kisheria na upeo

Ondoleo hili limetolewa chini ya Notisi ya Serikali Na. 520 na 522 ya 1995 inayosamehe Ushuru wa forodha na Ushuru wa Bidhaa pekee.

 

Sifa za Gari Linalostahili Msamaha

Ili gari lililoingizwa nchini kustahili msamaha huu, lazima:

a. Liwe halijazalishwa miaka 10 au zaidi kabla ya kuingizwa nchini.

b. Isipokuwa kwa Wabunge, gari hilo lisizidi uwezo wa injini wa 3000cc.

 

Masharti na Taratibu za Kuomba Msamaha

Afisa wa umma anayetaka kunufaika na msamaha huu anatakiwa kuwasilisha maombi katika ofisi ya forodha akiwa na nyaraka zifuatazo:

a. Barua ya utambulisho kutoka kwa mwajiri.

b. Uthibitisho wa mshahara wa hivi karibuni.

c. Barua ya uteuzi au ya kupandishwa cheo.

d. Fomu za maombi zilizojazwa kikamilifu, zikiwa na picha moja ya pasipoti kwenye kona ya juu kulia ya ukurasa wa kwanza.

e. Kitambulisho cha mfanyakazi.

f. Nyaraka za uingizaji wa gari (mfano: Hati ya Usafirishaji wa Mizigo (bill of lading), Taarifa ya Kusafirisha Mizigo kwa Njia ya Barabara (road consignment notice), ankara n.k.) kwa magari yaliyoingizwa kutoka nje, au risiti, mkataba wa mauzo, nyaraka za zabuni n.k. kwa magari yaliyopatikana ndani ya nchi.

g. Risiti ya TRA au stakabadhi za benki kama ushahidi wa malipo ya kodi endapo mwombaji alipata msamaha kama huo hapo awali.

 

Kumbuka: Msamaha huu unatatumika mara moja ndani ya miaka minne, ukihitaji msamaha mwingine baada ya miaka minne utalazimika kulipia kodi uliyosamehewa kwenye msamaha uliopita