Emblem TRA Logo
Usajili wa vyombo vya Moto

Usajili: Unamaanisha Usajili wa Chombo cha Moto chini ya Sehemu ya I ya Sheria ya Usalama Barabarani.

 

Kodi ya Usajili: Inamaanisha kodi inayotozwa na Sehemu ya II ya Sheria ya Vyombo vya Moto (Usajili na Uhamisho).

 

Uhamisho: Unamaanisha muamala wowote ambapo mali, au maslahi yoyote katika mali, chombo cha moto huhamishwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine iwe kwa mujibu wa uuzaji, rehani au mpangilio mwingine wa aina yoyote, na iwe uhamisho huo ni kwa malipo ya thamani au vinginevyo.

 

Kodi ya uhamisho: Kodi inayotozwa na Sehemu ya III ya Sheria ya Vyombo vya Moto (Usajili na Uhamisho).

 

Pikipiki: Ni chombo cha moto chenye magurudumu chini ya manne, ambacho uzito wake bila mzigo hauzidi kilogramu mia nne.

 

Chombo cha Moto: Ni chombo chochote kinachojiendesha chenyewe kilichokusudiwa au kubadilishwa kwa matumizi ya barabarani na kinajumuisha mitambo ya kihandisi.

 

Maombi ya Usajili

Maombi ya usajili wa Vyombo vya Moto au trela yatafanywa kwa fomu maalum na mmiliki wa Chombo cha Moto au trela kwenda kwa Mamlaka na yataambatanishwa na ada zilizowekwa.

 

Kodi ya Usajili

Kodi ya usajili wa chombo cha moto Inatozwa, kukusanywa na kulipwa kwa kiwango kilichowekwa katika Jedwali la Kwanza la Sheria.

 

Aina za Usajili wa Vyombo vya Moto

Usajili wa Kwanza wa Chombo cha Moto: Ni wakati chombo cha moto kinaposajiliwa kwa mara ya kwanza baada ya kuingizwa nchini au kuwekwa katika kundi jipya katika Mfumo wa Msajili Mkuu wa Vyombo vya Moto (CMVRS).

 

Usajili Unaofuata au Mwingine: Hii inajumuisha aina nyingine za usajili kama vile:

  • Mabadiliko ya Matumizi 
  • Mabadiliko ya Rangi 
  • Mabadiliko ya Taarifa za Chombo 
  • Uhuishaji wa Taarifa 
  • Marekebisho ya Hati za Umiliki 
  • Kufuta Usajili wa Chombo, n.k.

Leseni na usajili wa vyombo vya moto kwa mara ya kwanza

Ada ya Leseni ya Chombo cha Moto kwa mara ya kwanza hutegemea uwezo wa injini ya gari (CC)

Uwezo wa Injini (cc)Ada
501 – 1500cc Sh.200,000/-
1501 – 2500ccSh. 250,000/-
2501 na ZaidiSh. 300,000/-
Ada ya leseni ya  pikipiki au bajajiSh. 50,000/-
Ada ya Leseni ya Chombo cha Motokwa Vyombo vya moto vinavyotumia injini ya nishati ya umeme

Micro Hybrid with capacity 5< Kw

Shs. 50,000/-

Mild/semi Hybrid with capacity 6-30 Kw

Shs. 200,000/-

Full Hybrid  with capacity 31-40 Kw 

Shs. 250,000/-

Plug in Hybrid with capacity 41-90 Kw 

Shs. 300,000/-

Ada ya Usajili  wa Chombo cha moto
Magari yote bila kujali CCSh. 250,000/-

Vyombo vinginevyo

Sh. 250,000/=
Ada ya usajili kwa namba BinafsiSh.5,000,000- kwa miaka 3

Ada maalumu ya usajili ambayo kwa kutumia ni nyongezanamba ya ada ya usajili wa gari

Sh. 500,000/=
Ada ya Usajili Chombo chaMoto kwa Vyombo vya moto vinavyotumia injini ya nishati ya umeme

Magari ya kutumia nishati ya umeme chini ya Kilowati 5

Shs. 95,000/=

Magari ya kutumia nishati ya umeme chini ya Kilowati 6 mpaka 30,                     kilowati  31-40 , kilowati 41-90

Shs. 250,000/=

 

Usajili wa vyombo Moto

DarajaKodi ya Usajili
Daraja la 1 :EV za Nguvu za chini (Chini ya 50 kWh)95,000/=
Daraja la 2 : EV za nguvu ya kati (50.1 – 100 Kwh)250,000/=
Daraja la 3: EV za nguvu za juu (100.1-200kWh)250,000/=
Daraja la 4: Utendaji/EV za Ubora wa Juu(Zaidi ya KwH 200)250,000/=

Tozo ya Mwitikio wa VVU (HIV Response Levy)

Kodi ya Usajili na Ada ya Leseni & Tozo Mpya Iliyoanzishwa chini ya Kifungu kipya cha 5A kimeanzishwa, kikileta tozo mpya inayojulikana kama Tozo ya Mwitikio wa VVU (HIV Response Levy) kwenye usajili wa kwanza wa vyombo vya moto, ambayo itatozwa kwa kiwango kilichowekwa katika Jedwali hapo chini.

Aina ya Chombo/Ujazo wa Injini

Tozo (TZS)

Vyombo vya Moto 
(i) 0 cc-1000cc

50,000

(ii) 1001cc -1500cc

100,000

(iii) 1501cc -2500cc

150,000

(iv) 2501cc- na kuendelea

200,000

Mitambo (Magreda, Matrekta, Fork Lifts) n.k.

250,000

Uhamisho wa Chombo cha Moto na Kodi ya Uhamisho

Kodi ya Uhamisho 

Kodi ya uhamisho inatozwa, na kukusanywa kwa kiwango maalum.

Uhamisho unachukuliwa kuwa umekamilika ikiwa:

  • Unaambatana na uwasilishaji wa milki ya Chombo cha Moto, tarehe ambayo uwasilishaji huo unafanyika.
  • Umeidhinishwa au unahitajika kuidhinishwa kwenye kadi yoyote ya usajili au daftari lililotolewa au linalotunzwa kwa mujibu wa masharti ya Sheria ya Usalama Barabarani, tarehe ambayo uidhinishwaji huo unafanyika, kutegemeana na tarehe ipi itakayotangulia.

Kuhamisha umiliki wa chombocha moto

Ada ya gariSh 50,000/-
Ada ya pikipikiSh. 27,000/-
Ada ya Nakala ya kadi (Duplicate)
GariSh. 50,000/=
Pikipikimatatu(Bajaj) ya magurudumuSh. 30,000/=
PikipikiSh. 20,000/=.
Leseni za Udereva
Ada ya leseni kila baada ya miaka mitanoSh 70,000/-
Ada ya majaribio ya uderevaSh. 3,000/=
Leseni ya mudaya uderevaSh 10,000/-

 

Jedwali la Michakato, na Mahitaji,

MchakatoMahitaji 

Mabadiliko ya Umiliki

(Mtu Binafsi)

· Mkataba wa mauzo

· Hati ya zawadi

· Hati ya dhamana (Mortgage deed)

· EFD ya Wakili

· Barua ya maombi

· Nambari ya Utambulisho wa Mlipaji Kodi (TIN) kwa Mnunuzi

Mabadiliko ya Umiliki
(Kampuni Ndogo)

· Mikataba ya mauzo

· Risiti ya EFD ya mauzo

· EFD za Wakili

· Barua ya maombi

· Nambari ya Utambulisho wa Mlipaji Kodi (TIN) kwa Mnunuzi

Kwa Hali ya Wauzaji Wasiopatikana

· Mikataba ya mauzo iliyothibitishwa na Wakili

· Cheti cha Umiliki (Affidavit of Ownership)

· Risiti ya EFD kutoka kwa Wakili

· Uthibitisho kutoka BRELA (kwa Kampuni Ndogo)

· Barua ya maombi

Kufuta Usajili

· Ajali za moto, Magari yaliyoharibika kabisa (Scrapped), Kuibwa

· Uhamisho nje ya nchi (Export)

Kuzuia/Kuondoa KuzuiaKuzuia magari kwa ombi la mmiliki
Mabadiliko ya Umiliki
(kwa Kampuni Ndogo)

· Mikataba ya mauzo

· Risiti ya EFD ya mauzo

· EFD za Wakili

· Barua ya maombi