Emblem TRA Logo

Shirika la hisani ni taasisi iliyosajiliwa nchini Tanzania yenye lengo kuu la kuboresha ustawi wa jamii zenye uhitaji kwa kutoa huduma kama elimu bure, huduma za afya, pamoja na ujenzi au ukarabati wa miundombinu. Aidha, shirika hilo linapaswa kuwa na cheti kutoka TRA kinacholitambua rasmi kuwa ni shirika la hisani.

 

Vigezo vya Kutambuliwa kama Shirika la hisani kwa Madhumuni ya Kodi

 

Shirika la hisani ni taasisi iliyosajiliwa nchini Tanzania yenye lengo la kuboresha ustawi wa jamii kwa kutoa huduma kama elimu bure, huduma za afya, maji safi, au ujenzi na ukarabati wa miundombinu. Ili kutambuliwa kwa madhumuni ya kodi, shirika linapaswa kufanya shughuli zake kwa manufaa ya umma na si kwa lengo la kupata faida binafsi. Shirika linapaswa kuwa wazi kwa umma au kundi maalum lenye lengo la pamoja, kama kusaidia wajane, watoto au watu wenye ulemavu. Mapato au ziada yoyote itakayopatikana haitakiwi kugawanywa kwa wanachama, viongozi au waanzilishi, bali itumike kuendeleza shughuli za hisani za shirika. 

 

Shirika lazima liwe na uamuzi halali (ruling) kutoka kwa Kamishna unaothibitisha kutambuliwa kwake kama shirika la hisani kwa madhumuni ya kodi.

 

Maombi ya Kutambuliwa kama Shirika la hisani

 

Maombi yanapaswa kuwasilishwa kwa Meneja wa Mkoa katika mkoa ambako shirika limesajiliwa, yakiwa yameambatanishwa na cheti cha usajili, katiba na taarifa ya utekelezaji wa shughuli, barua ya utambulisho kutoka kwa Mkuu wa Wilaya wa eneo husika, cheti cha TIN, na taarifa za fedha za miaka mitatu iliyopita.

 

Kutambuliwa kama shirika la hisani na Kamishna Mkuu wa TRA hakumaanishi moja kwa moja kupata msamaha wa kodi ya mapato. Shirika bado lina wajibu wa kutekeleza majukumu yake ya kodi, ikiwemo kuwasilisha ritani  za kodi kwa mujibu wa sheria.