Faida ya mtaji kutokana na kupata riba katika ardhi na majengo.
Upatikanaji wa riba katika ardhi na majengo
Mtu anayepata riba katika ardhi au jengo atachukuliwa kama anapata mali pindi atakapoacha kupata riba hiyo ikiwa ni pamoja na wakati mali hiyo inapouzwa, inapobadilishwa, inapobadilishwa umiliki, inapogawanywa, inapobatilishwa, inapokombolewa, inapoteketezwa, au inaposalimishwa na katika suala la riba ya mali hiyo uwepo wake unapokoma, mara kabla ya kuwepo ukomo wa mali hiyo.
Sheria ya Kodi ya Mapato inamtaka mtu anayepata faida kutokana na kupata riba katika ardhi au majengo yaliyo katika Jamhuri ya Muungano, kulipa kodi ya mapato kwa awamu moja.
Awamu Moja ya Malipo ni nini?
Kodi ya mapato inayolipwa kwa awamu moja kutokana na kupata riba katika ardhi au majengo ni kiasi cha kodi kinacholipwa mara moja kabla umiliki haujahamishwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine. Msajili wa Hatimiliki hatasajili uhamishaji huo pasipo kuonyesha hati kutoka Mamlaka ya Mapato inayothibitisha kuwa malipo ya awamu moja yamelipwa au hayalipwi. Muuzaji anatakiwa kutoa taarifa kuhusu uhamishaji wa riba ya ardhi au jengo.
Viwango Vinavyotumika
(a) 10% ya faida kwa mkazi;
(b) 30% ya faida kwa mtu asiyekuwa mkazi
(c) 3% ya thamani ya aridhi au jengo, kwa muuzaji wambaye hana nyaraka ambazo zinaeleza uhalali wa gharama za mali.
Hata hivyo, Sheria Kodi ya Mapato inaeleza kuwa mlipaji kwa awamu atastahili punguzo la kodi kwa mwaka wa mapato wa kiasi sawa na kodi ya mapato iliyolipwa kwa awamu moja kwa mwaka wa mapato.
Misamaha ya Kodi
a) Iwapo makazi yamekuwa yakimilikiwa na mtu kwa miaka mitatu au zaidi na mtu huyo amekuwa akiishi humo mfululizo au kwa vipindi vya jumla ya miaka mitatu au zaidi; na wakati wa mauzo faida haizidi Shilingi 15,000,000.
b) Ardhi inayomilikiwa na mtu yenye thamani ya soko isiyozidi shilingi 10,000,000 wakati wa mauzo na imekuwa ikitumika kwenye shughuli za kilimo kwa angalau miaka miwili kati ya mitatu kabla ya kuuzwa.
c) Hisa zilizoorodheshwa kwenye soko la hisa la Dar-es- Salaam zinazomilikiwa na mkazi au asiye mkazi kwa kiwango kisichozidi 25% ya umiliki wa kampuni.
Faida itokanayo na uuzaji wa rasilimali Inakokotolewaje?
Faida ya Mtaji = Bei ya Uuzaji (au Mapato ya Mauzo) − [Bei ya Ununuzi + Gharama za Ununuzi + Gharama za Maboresho + Gharama za Matengenezo na Ukarabati + Gharama za Uuzaji + Gharama Nyingine Zinazoruhusiwa].
Je, matumizi ya utekelezaji ni nini?
Gharama za utambuzi wa mauzo ni gharama anazotumia mtu katika mchakato wa kuuza au kuhamisha umiliki wa mali. Gharama hizi zinajumuisha matumizi yanayohusiana moja kwa moja na uuzaji au uhamishaji wa mali hiyo, kama vile ada za kisheria, kamisheni za madalali au mawakala, ada za mnada, gharama za kuthamini mali, gharama za matangazo, kodi na tozo za uhamisho, ada za usajili, ada za wapimaji wa ardhi, pamoja na gharama nyingine zozote zinazotumika mahsusi kwa ajili ya kukamilisha mauzo au uhamisho wa mali hiyo.
Kodi ya Faida ya Mtaji katika Upatikanaji (Uuzaji) wa Dhamana
Dhamana ni nini?
Ni mali yoyote inayouzika (mali za uwekezaji za aina yoyote). Dhamana kwa ujumla zimegawanyika katika makundi yafuatayo:
- Dhamana za hisa zisizo za kudumu (k.m. Hisa za kawaida na hisa maalum za upendeleo)
- Dhamana za madeni, (k.m. dhamana na hati za kurejeshewa malipo
- Dhamana zilizozalishwa (k.m., Mkataba wa kibiashara kwa mauzo ya baadae, Mkataba wa kuuza mali kwa bei ya makubaliano kwa kuwasilisha na kulipwa baadaye, Mkataba wa mauziano usiokuwa na masharti na Biashara ya mali kwa mali).
Kodi ya Faida Halisi Itokanayo na Kuuza Dhamana
Faida halisi itokanayo na kuuza dhamana inachukuliwa kama mapato ya uwekezaji yatakayojumuishwa katika kujua jumla ya mapato ya mtu katika mwaka wa mapato kama inavyoelekezwa na Sheria ya Kodi ya Mapato ya mwaka 2004. Mapato ya jumla ya asasi yanakokotolewa katika kiwango cha 30% ilhali viwango vya kodi kwa mkazi vitahusika katika mapato ya jumla ya mkazi mmojammoja.
Faida Gani Zinatokana na Mauzo ya Mali za Uwekezaji?
Faida kutokanayo na mauzo ya mali ya uwekezaji ni ziada bei ya soko dhidi ya gharama ya mali hiyo.
Faida halisi kutokana na mauzo ya mali za uwekezaji ni jumla ya faida zote kutokana na mauzo ya mali za uwekezaji ukiondoa:-
- Jumla ya hasara zote katika kuuza mali za uwekezaji;
- Hasara zozote ambazo hazijapunguzwa katika kipindi cha mwaka; na
- Hasara zozote za mwaka uliopita ambazo hazijapunguzwa.
Gharama ya mali ni nini (Dhamana)?
Gharama ya mali ni jumla ya gharama zilizotumika katika kupata mali, ikiwa ni pamoja na:
Dhamana Zilizoondolewa kwenye Orodha
Hisa zilizoorodheshwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam ikiwa tu hisa hizo zinamilikiwa na raia wa ndani au raia wa nje anayemiliki chini ya 25% ya hisa za kampuni husika.
Ukomo katika Hasara za Vitegauchumi
Iwapo mtu anapata hasarra kutokana na uwekezaji wowote inawezekana kufidia mapato kutoka kwenye uwekezaji mwingine na haiwezi kufidia mapato kutoka kwenye biashara yoyote.
Ukomo katika Faida za Mtaji
Kama mtu atapata hasara anapouza mali ya uwekezaji, inaweza kufidia faida tu kutokana na kuuza mali nyingine za uwekezaji.
Hasara za uwekezaji kutoka nje unaweza kufidia mapato ya uwekezaji toka nje tu, hasara za mauzo ya mali za uwekezaji zinaweza kufidiwa tu na mauzo ya mali za uwekezaji kutoka nje.
Habari & Matukio
TRA YAKUTANA NA UJUMBE WA SHIRIKA LA FEDHA DUNIANI - IMF