CTI NA TRA WAKUTANA KUTAFUTA SULUHISHO LA BEI YA SARUJI
15 September, 2026
Uongozi wa Shirikisho la Wenye Viwanda Nchini Tanzania (CTI) na Menejimenti ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutafuta suluhisho la pamoja kuhusu kupanda kwa bei ya Saruji nchini.
Akizungumza katika kikao hicho kilichifanyika Septemba 14, 2026 jijini Dar es Salaam Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Yusuph Juma Mwenda amesema wameamua kukutana na Shirikisho hilo ikiwa ni sehemu ya kutafuta namna ya kupunguza bei ya Saruji ambayo imelalamikiwa kupanda kwa kiasi kikubwa katika siku za karibuni.
Kamishna Mkuu Mwenda amesema jukumu la TRA ni kuwezesha biashara na uwekezaji nchini hivyo hatua inazochukua ni kuhakikisha mazingira ya biashara nchini yanaendelea kuwa katika hali nzuri na kuwanufaisha wafanyabiashara na watumiaji wa bidhaa zinazozalishwa.
"Tumeanza kwa kukutana na Shirikisho la wenye Viwanda ili tutafute suluhisho la pamoja la changamoto ya kupanda kwa bei ya Saruji lakini nitakutana na wamiliki wa viwanda mmoja mmoja ili kutafuta suluhisho la kudumu la changamoto ya bei" amesema Bw. Mwenda.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CTI Bw. Hussein Sufiani Ali amesema tayari walishaanza kutafuta suluhusho la kupanda kwa bei ya Saruji kwa kutafuta chanzo chake ambacho walikuta kuwa ni kupungua kwa uzalishaji wa madini yanayotumika kuzalisha saruji yanayofahamika kama 'Klinca'.
Amesema kufuatia kikao walichifanya na TRA kitawezesha kuendelea kufanya ufuatiliaji ili kupata suluhisho la kudumu.