BIDHAA BANDIA NA MAGENDO ZINAATHIRI BIASHARA NA MAPATO YA SERIKALI - MAKAMU WA RAIS NDEJEMBI
04 September, 2026
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, amekemea vikali uingizaji wa bidhaa bandia nchini kwa njia za magendo, akieleza kuwa vitendo hivyo vinadhoofisha ushindani wa haki katika biashara, vinaikosesha Serikali mapato stahiki na kuhatarisha afya na usalama wa Watanzania.
Mhe. Ndejembi ameyasema hayo Septemba 2, 2026, akiwa Mgeni Rasmi katika Tuzo za Rais za Mzalishaji Bora zilizofanyika katika Ukumbi wa Superdome, Masaki jijini Dar es Salaam, ambapo amesisitiza umuhimu wa wadau mbalimbali kushirikiana katika kukabiliana na biashara ya bidhaa bandia na magendo ili kulinda wazalishaji wa ndani, kuongeza mapato ya Serikali na kuhakikisha wananchi wanapata bidhaa salama na zenye ubora.
Wazalishaji wa bidhaa mbalimbali nchini walitunukiwa tuzo kwa kutambua na kuthamini mchango wao katika kukuza uzalishaji wa ndani, kuongeza ajira, kuchochea ukuaji wa uchumi na kuchangia maendeleo ya Taifa.