SERIKALI YA CHINA YAISAIDIA TANZANIA KUONGEZA WIGO WA KODI
13 November, 2025
Katika kuimarisha ushirikiano wa muda mrefu kati ya Tanzania na China, Serikali ya China kupitia Ubalozi wake nchini Tanzania imetoa vishkwambi kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), vitakavyotumika kusajili walipakodi moja kwa moja kutoka kwenye maeneo yao ya biashara, hatua inayolenga kupanua wigo wa walipakodi na kuongeza Mapato ya Serikali.
Akizungumza wakati wa makabidhiano ya vifaa hivyo yaliyofanyika Novemba 12, 2025 jijini Dar es Salaam kati ya Balozi wa China, Mhe. Chen Mingjian na Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Yusuph Juma Mwenda, Kamishna Mkuu Mwenda amesema msaada huo utaongeza ufanisi wa TRA katika kuwafikia wananchi na kurahisisha usajili wa walipakodi wapya.
Amesisitiza kuwa kadri idadi ya walipakodi inavyoongezeka, mzigo wa kodi unapungua kwa mtu mmoja mmoja na mapato ya Taifa yanakuwa imara zaidi, hivyo ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kujisajili watakapofikiwa.
Kwa upande wake, Balozi Mhe. Chen Mingjian amesema msaada huo ni sehemu ya kuimarisha ushirikiano kati ya China na Tanzania, akiongeza kuwa wapo wawekezaji wengi wa China wanaonufaika na huduma za TRA, hivyo ni muhimu kuendelea kuunga mkono taasisi hiyo muhimu kwa maendeleo ya Uchumi wa Tanzania.
Habari Mpya
IDRAS ITAONGEZA WIGO WA KODI NA KUSIMAMIA USAWA – CG MWENDA
MKUTANO WA TATHMINI YA UTENDAJI WA NUSU MWAKA
TRA YAKUSANYA TRILIONI 4.13 MWEZI DESEMBA PEKEE
IDRAS KULETA MAPINDUZI YA KIUTENDAJI TRA