Emblem TRA Logo

CG MWENDA AKUTANA NA DCG WA RWANDA, WAKUBALIANA KUWEZESHA BIASHARA MIPAKANI

07 October, 2026

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Yusuph Juma Mwenda amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato nchini Rwanda (RRA) 
Dkt. Murasi Innocente na kukubaliana kuendelea kuwezesha biashara mipakani.

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Oktoba 07, 2026 jijini Arusha kunakoendelea mkutano wa Chama cha Wasimamizi wa Kodi wa Jumuiya ya Madola (CATA) Kamishna Mkuu Mwenda amesema Tanzania na Rwanda zinapakana na iwapo zitashirikiana kuwezesha biashara mipakani wataweza kukomesha bidhaa za magendo baina ya nchi hizo.

Amesema Tanzania na Rwanda zimekuwa na uhusiano mzuri wa muda mrefu hivyo wataendelea kuboresha zaidi mazingira ya kodi mipakani kwa lengo la kuwezesha biashara.

Kwa upande wake Naibu Kamishna Mkuu wa RRA Dkt. Murasi Innocente amesema Mamlaka hiyo itaendelea kuwa na uhusiano mzuri na TRA na kushirikiana nao katika masuala ya ulinzi wa mipaka kwa kuzuia magendo na kuboresha mazingira ya kodi baina ya nchi hizo mbili.