RAIS WA CATA, DKT. ABU TARIQ JAMALUDDIN, AWASILI ARUSHA TAYARI KUSHIRIKI MKUTANO
06 October, 2026
Rais wa CATA, Dkt. Abu Tariq Jamaluddin, amewasili jijini Arusha kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 46 wa CATA unaofanyika nchini Tanzania. Kuwasili kwake ni miongoni mwa hatua zinazoendelea kuelekea kuanza kwa mkutano huo unaowakutanisha viongozi na wawakilishi kutoka nchi mbalimbali wanachama wa CATA.
Dkt. Jamaluddin amepokelewa na mwenyeji wake, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Yusuph Juma Mwenda, ambaye amemkaribisha nchini Tanzania na jijini Arusha kwa ajili ya kushiriki mkutano huo muhimu.
Mkutano wa 46 wa CATA unalenga kuwakutanisha wataalamu na viongozi wa mamlaka za mapato kutoka nchi wanachama kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali yanayohusu usimamizi wa mapato na namna teknolojia inavyoweza kuimarisha ufanisi katika ukusanyaji wa kodi.
Mkutano huo unaofanyika kuanzia tarehe 5 hadi 9 Oktoba 2026 jijini Arusha, unafanyika chini ya kaulimbiu inayosisitiza matumizi ya teknolojia katika kuboresha ufanisi wa ukusanyaji wa mapato.
Habari Mpya
CG MWENDA: HAKUNA BIASHARA ITAKAYOFUNGWA KWA SABABU YA KODI
TANZANIA NA MALAWI KUENDELEA KUBORESHA HUDUMA ZA KODI MIPAKANI