Kwa kutumia tovuti hii ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), unakubaliana na kufuata vigezo na masharti yafuatayo.
Matumizi ya Tovuti
Tovuti hii inatumika kwa ajili ya kutoa taarifa za jumla na kupata huduma za TRA. Unakubali kuitumia kwa madhumuni halali na kwa namna ambayo haiingilii haki za wengine wala kuizuia matumizi yao ya tovuti hii.
Hairuhusiwi kutumia vibaya tovuti hii kwa kuiwekea virusi au programu hasidi, kujaribu kupata taarifa zisizoruhusiwa bila idhini, au kuingilia utendaji wake wa kawaida.
Usahihi wa Taarifa
TRA inafanya juhudi za kuhakikisha kuwa taarifa zilizopo kwenye tovuti hii ni sahihi na zinasasishwa mara kwa mara. Hata hivyo, maudhui yaliyomo kwenye tovuti yanatolewa kama mwongozo wa jumla tu na yanaweza kubadilika wakati wowote bila taarifa.
Watumiaji wanashauriwa kutafuta mwongozo rasmi kutoka kwa TRA pale inapohitajika, hasa katika masuala yanayohusu majukumu ya kisheria au kifedha.
Mali Miliki
Maudhui yote yaliyomo kwenye tovuti hii yakiwemo maandishi, nembo, au michoro ya kubuni ni mali ya TRA isipokuwa itakavyoelezwa vinginevyo. Hairuhusiwi kunakili, kuzalisha au kusambaza kwa madhumuni ya kibiashara bila idhini ya maandishi kutoka kwa TRA.
Viungo vya Nje
Tovuti hii inaweza kuwa na viungo vinavyoelekeza kwenye tovuti au mifumo ya nje ya TRA. TRA haihusiki wala kuidhinisha maudhui ya tovuti hizo na wala haihusiki na uendeshaji au upatikanaji wake.
Ukomo wa Dhima
TRA haitawajibika kwa hasara yoyote au uharibifu unaotokana na matumizi au kushindwa kutumia tovuti hii au maudhui na taarifa zilizomo ndani yake.
Mabadiliko ya Sheria na Masharti
TRA ina haki ya kusasisha au kurekebisha vigezo na masharti haya wakati wowote. Kuendelea kutumia tovuti hii kunamaanisha kukubaliana na mabadiliko yoyote yanayofanywa au yatakayofanywa.
Muongozo wa Sheria
Vigezo na masharti haya yataongozwa na kutafsiriwa kwa mujibu wa sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.