Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inaheshimu faragha yako na imejidhatiti katika kulinda taarifa zako binafsi. Taarifa hii ya faragha inaelezea jinsi tunavyokusanya, kutumia, na kulinda taarifa zako unapotumia tovuti na huduma zetu.
Taarifa Tunazokusanya
Tunaweza kukusanya taarifa binafsi ambazo unatupatia moja kwa moja au vinginevyo. Taarifa hizo ni kama vile jina lako kamili, taarifa za mawasiliano, namba ya usajili wa biashara, kadi ya mpiga kura na maelezo ya pasi ya kusafiria (passport), namba ya utambulisho wa taifa (NIN), tarehe ya kuzaliwa, jinsia, taarifa za kibaolojia (picha, alama za vidole, na sahihi), taarifa ya vyombo vya moto vilivyosajiliwa au visivyosajiliwa, maelezo ya uingizaji na uuzaji wa bidhaa nje ya nchi, namba ya utambulisho wa mlipakodi (TIN), maelezo ya mapato na namba za akaunti ya benki, kumbukumbu za malipo, madeni ya kodi, na madai ya marejesho ya kodi, maelezo ya biashara na hali ya ajira, ritani za kodi na taarifa nyingine yoyote inayowasilishwa kupitia fomu zetu za mtandaoni au huduma zetu.
Pia, tunaweza kukusanya taarifa chache za kiufundi kama vile anwani yako ya IP, aina ya kivinjari, na kurasa ulizotembelea, ili kutusaidia kuboresha tovuti yetu.
Jinsi Tunavyotumia Taarifa Zako
Tunatumia taarifa zilizokusanywa katika:
- Kutoa na kuboresha huduma zetu.
- Kujibu hoja na maombi yako.
- Kuchakata maombi na miamala mbalimbali.
- Kutii matakwa ya kisheria na kikanuni.
- Kuimarisha usalama na utendaji wa mifumo yetu.
Utoaji wa Taarifa
TRA haiuzi wala kutoa taarifa zako binafsi kwa mtu, watu au taasisi nyingine kwa madhumuni ya kibiashara. Taarifa zako zinaweza kutolewa kwa taasisi za serikali zilizoidhinishwa au watoa huduma pale inapohitajika, na kwa mujibu wa sheria na kanuni husika.
Usalama wa Taarifa
Tunachukua hatua madhubuti za kiufundi na kiutawala ili kulinda taarifa zako binafsi dhidi ya upotevu, matumizi mabaya, upatikanaji au mabadiliko yoyote yasioidhinishwa.
Viunganishi vya Nje
Tovuti yetu inaweza kuwa na viunganishi vya tovuti nyingine za nje ya TRA. TRA haihusiki na taratibu za faragha au maudhui ya tovuti hizo. Tunakuhimiza kupitia sera zao za faragha.
Wajibu Wako
Tafadhali hakikisha kuwa taarifa unazotoa ni sahihi, na pia unahifadhi na kulinda usalama wa neno lako la siri unalotumia kuingilia kwenye mifumo yetu.
Wasiliana Nasi
Ikiwa una maswali au duduku kuhusu Taarifa hii ya faragha au jinsi taarifa zako zinavyoshughulikiwa, tafadhali wasiliana na TRA kupitia njia zetu rasmi za mawasiliano.