1.0      UTANGULIZI

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeanzisha mfumo ambao utaboresha ukusanyaji wa mapato yatokanayo na ada za magari. Mfumo umeanza kutumika rasmi kuanzia tarehe 9 Agosti 2013.

Kutokana na kuanzishwa kwa mfumo huu, malipo yote ya kodi za magari yatafanywa kwa njia ya mtandao kwa maana ya kutumia simu za kiganjani, benki na wakala wa Maxmalipo. Hii itawawezesha walipakodi kulipa ada za magari bila kufika katika ofisi za TRA isipokuwa kwa ajili ya kuchukua kadi za magari (stika).

Mfumo huu utatumika kulipa ada za mwaka za magari, ada za kubadilisha umiliki wa magari na ada nyingine zinazohusu usajili wa magari.

2.0      FAIDA ZA MFUMO

Mfumo huu umeanzishwa kutokana na faida nyingi kama:

  1. Mfumo huu ni rahisi kuutumia na utapunguza misongamano isiyo ya lazima katika ofisi za Mamlaka ya Mapato na benki na hivyo kumwezesha mlipakodi kulipa ada ya gari lake akiwa mahali popote nchini.
  2. Mfumo huu una panua wigo wa njia za kulipa kodi kwa hiyo unampa mlipakodi uhuru wa kuchagua njia ambayo anaona ni rahisi kutumia kutokana na mazingira atakayo kuwamo.
  3. Vilevile kwa kutumia utaratibu huu mlipakodi anaweza kuhakiki kiwango cha ada ya gari anachotakiwa kulipa na hivyo kuepuka udanganyifu unaofanywa na watu wasio waaminifu.
  4. Mfumo huu ni salama kwani kuna uhakika kwamba malipo yote ya kodi yanakwenda Benki Kuu kwani unahusu mawasiliano ya mtandao bila kuhusisha mtu.
  5. Kwa upande mwingine mfumo huu unaiwezesha TRA kukusanya kodi kwa gharama nafuu.

3.0      UTARATIBU WA KULIPA:

  1. Kufahamu kiwango cha kodi. Tuma ujumbe wenye neno “Kadiria” au “Assess” acha nafasi andika namba za gari mfano KADIRIA T765AAU kwenda namba 15341.  
  2. Kujisajili: Tuma ujumbe wenye neno; “sajili” acha nafasi na kuandika namba ya gari husika mfano SAJILI T765AAU. Tuma ujumbe huo kwenda namba 15341. Baada ya hapo mlipakodi atapata ujumbe wa namba ya kumbukumbu ya malipo (Reference number).
  3. Fanya malipo kwa kutumia TIGOPESA, M-PESA, AIRTELMONEY, Benki ya CRDB au wakala wa MAXMALIPO kwa kutumia namba ya kumbukumbu uliyopata. Namba za Kampuni ni TIGO-PESA na M-PESA ni 800600. AIRTEL-MONEY ni TRAMAGARI.
  4. Kuchukua kadi: (stika ya gari): nenda katika ofisi yoyote ya TRA ukiwa na namba ya kumbukumbu uliyoitumia kufanya malipo.

Zingatia.

Hakuna wakala atakayeruhusiwa kuchukuwa kadi ya gari hivyo bali mmiliki wa gari ndio pekee atakayeruhusiwa kuchukua kadi ya gari. Ili kuweza kuchukua kadi ya gari, pamoja na kuwa na namba ya kumbukumbu mmiliki wa gari anatakiwa kuwa na kitambulisho chochote kama vile leseni ya udereva, kitambulisho cha mfuko wa hifadhi ya jamii, kitambulisho cha Taifa, kitambulisho cha mpiga kura au Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN).

Viwango vya ada za magari

SN

Ukubwa wa Injini

Ada

Ada ya ukaguzi wa vifaa vya Zimamoto

Jumla

1

0 – 500. cc

50,000/=

10,000/=

60,000/=

2

501- 1500.cc

150,000/=

20,000/=

170,000/=

3

1501- 2500.cc

200,000/=

30,000/=

230,000/=

4

Zaidi ya 2500.cc

250,000/=

40,000/=

290,000/=

 

Angalizo: Pikipiki zimesamehewa kulipa ada ya mwaka isipokuwa zinatakiwa kulipiwa ada ya ukaguzi wa vifaa vya zimamoto ambayo ni TSh 10,000/=

Kwa wale ambao wanahitaji kubadilisha umiliki wa magari, kuomba nakala ya gari na kubadilisha taarifa za gari wanatakiwa kufika katika ofisi ya TRA ili kufanyiwa makadirio pamoja na kuingiza taarifa katika mfumo wa magari.

Kwa ufafanuzi zaidi kuhusu jinsi mfumo unavyofanya kazi, tafadhali wasiliana na kituo cha Huduma kwa Wateja kwa kupiga simu za bure:-

·         0786 800 000 kwa watumiaji wa Airtel

·         0713 800 333 kwa watumiaji Tigo

·         0800110016 kwa watumiaji wa Vodacom na TTCL

The motor vehicle licence fee is charged on first registration of a motor vehicle  are based on the size of the engine as shown in the table below:

This fee shall not apply to Motorcycle or a tricycle commonly known as Bajaji

         Cubic capacity (cc)

             Fee

0 cc - 500 cc

Tshs 50,000/=

501 cc – 1,500cc

Tshs 200,000/=

1,501 cc – 2,500cc

Tshs 250,000/=

2,501cc and above

Tshs 300,000/=

Motor vehicle transfer tax is payable when a vehicle changes ownership from one person to another. Tax on transfer is payable by the transferee and Stamp Duty on the sale of asset is paid by the seller. The taxes are paid through the bank.

Motor Vehicle Transfer Tax

Motor Vehicle transfer fees

Tshs 50,000/=

Motor cycle transfer fees

Tshs 27,000/=

Fee for Duplicate Card

 

Motor Vehicle 

Tshs 50,000/=

Tricycle (example Bajaji)

Tshs 30,000/=

Motor Cycle

Tshs 20,000/=